Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi kukataa kulaghaiwa na watu wachache kuipigia kura ya hapana wakati wa kura ya maoni katiba iliyopendekezwa kwani kufanya hivyo ni kurejesha nyuma taifa na vizazi vijavyo.
Rais ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wazee wa mkoa wa Dodoma ambapo pia amesema muda wa kuanza kampeni kuhusu kura za maoni bado hivyo ni vyema watu wakaheshimu sheria ya kura za maoni.
Rais Kikwete amesema jambo la msingi hivi sasa ni kuwaachia wananchi wenyewe waamue katika kura za maoni na si kuwalaghai kwa maneno ya watu wachache huku akiwataka watanzania kuisoma katiba hiyo pendekezi wao wenyewe na kuielewa ili wanapokwenda kupiga kura ya maoni wajue wanachokifanya.
Amewaasa watanzania kuipigia kura ya ndiyo katiba hiyo siku itakapofika. Ameongeza kuwa kura ya maoni inatarajiwa kufanyika ifikapo April 30 mwakani na kampeni zinatarajiwa kuanza Machi 30 hadi April 29. 2015.

0 comments