Showing posts with label mitaa. Show all posts
Showing posts with label mitaa. Show all posts

Monday, 19 March 2018

 Ofisa mradi wa Mbegu za Mahindi yanayostahimili  Ukame ya Wema 2109  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Bestina Daniel, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu hiyo katika Kijiji cha Kilemela kilichopo Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo jana. W a pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga na hao wengine ni viongozi mbalimbali katika wilaya hiyo.
 Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani, Kapilima George akizungumza.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, akitoa hutuba yake.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH,Shabani Hussein (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga  mbegu hizo kabla ya kuzindua shamba darasa. Katika ni Ofisa mradi wa Mbegu za Mahindi yanayostahimili  Ukame ya Wema 2109  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Bestina Daniel.
 Mwakilishi wa Kikundi cha Kikuki Malengo Group kutoka Kitongoji cha Amani, Othman Said Ally akikabidhiwa mbegu. Wa pili kulia ni Mtafiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Nikidadi Hamidu.
 Mkulima Julius Maina (kushoto), kutoka Kitongoji cha Zinga akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima Anaseli Macha kutoka Kijiji cha Kongo Kaya ya Yombo akikabidhiwa mbegu.
 Mkulima Ahazi Mwasibata akikabidhiwa mbegu.
 Hapa wakielekezwa namna ya upandaji wa mbegu hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, akizundua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu.
 Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani, Kapilima George na Ofisa Kilimo Ushirika na Umwagiliaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Mary Kisimbo wakipanda mbegu hiyo.
Mbegu hiyo ikipangwa katika shamba darasa eneo la Zinga.

Na Dotto Mwaibale, Bagamoyo

MKOA wa Pwani umepokea mbegu bora ya mahindi aina ya Wema kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa mkoani humo.

Akizungumza wakati akipokea mbegu hiyo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika jana katika Kijiji cha Kilemela Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo Mkuu wa wilaya hiyo Majid Mwanga alisema mbegu hiyo itasaidia kuondoa changamoto ya kupata mbegu bora kwa wakulima wilayani mwake.

"Niwashukuru wenzetu wa COSTECH na OFAB kwa kutukumbuka kwa kuendesha program hii ya kugawa mbegu bora ya mahindi katika mkoa wetu hususan kwenye wilaya yangu ya Bagamoyo" alisema Mwanga.

Alisema mradi huo utasaidia kuongeza ari ya kilimo cha mahindi kwenye wilaya hiyo na kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuhimiza kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha viwanda hapa nchini.

Aliwaomba wakulima hasa kwa wanavikundi waliopata mbegu hizo kuhakikisha wanayatunza mashamba darasa hayo kwa manufaa ya wakulima wote wa wilaya hiyo.

Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani Kapilima George alisema mbegu hizo zitaongeza mazao ya mahindi kwani licha ya kutumia mbegu zingine mkoa huo kwa mwaka jana ulipata tani 110.
  

Akizungumza kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.

Mtafiti  Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Nikidadi Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.

Ofisa mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kwa mkoa huo wametoa mbegu kilo 58 kwa ajili ya mashamba darasa katika wilaya ya Bagamoyo na Chalinze ambapo kwa wakulima mmoja mmoja wametoa kilo 42 pamoja na mbolea ya kupandia.

Tuesday, 13 March 2018

Na Jumia Travel Tanzania


Zimebaki takribani wiki tatu kabla ya sikukuu ya Pasaka kusherehekewa duniani kote, je umeshafahamu utakwenda kupumzika wapi? 

Pasaka ni miongoni mwa sikukuu zinazopendwa na watu wengi kwa sababu husherehekewa kwa takribani wiki moja. Wakati wa sherehe hizi watu huitumia fursa hiyo kwa kufanya mapumziko ya muda mfupi kabla ya kurejea kwenye shughuli zao za kila siku.

Katika kukusaidia sehemu za kwenda kutembelea sikukuu hii, Jumia Travel imekukusanyia hoteli tano za kuvutia zilizopo pembezoni mwa Tanzania ambazo unaweza kwenda kupumzika kipindi cha likizo hii fupi.

Lupita Island Lodge. Ni hoteli ya kuvutia na tulivu inayopatikana kwenye kisiwa kinachomilikiwa na mtu binafsi ndani ya ziwa Tanganyika. Hoteli hii ina kiwanja binafsi cha ndege na boti ambazo huwachukua wageni kutoka nchi kavu mpaka kisiwani. Hii ni sehemu ambayo unapaswa kwenda kwa ajili ya mapumziko kwa sababu hata namna ya muundo wa vyumba na mazingira yake yamewekwa kumpatia mtu utulivu na usiri akiwa mapumzikoni. Miongoni mwa shughuli za kuvutia ukiwa kisiwani hapa ni pamoja na kutembelea kijiji cha wavuvi, kutalii ziwani kwa kutumia boti na burudani za maonyesho ya kiasili kutoka kwa wanakijiji.  

Katuma Bush Lodge. Ikiwa inapatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi, hoteli hii imejengwa katika mtindo wa kuvutia na kustarehesha kwa kutumia mahema. Eneo hili linatoa wasaa mzuri kwa wateja kutembelea mbuga yenye mandhari nzuri ya uwanda wa Katisunga. Kwa kuongezea, ni sehemu nzuri kwa watalii ambao wangependa kutembelea na kujionea mazingira mapya tofauti na yale waliyokwishayazoea.  

Wag Hill Lodge & Spa. Hoteli ina mazingira tulivu na vifaa vya kisasa, sehemu kwa ajili ya michezo ya watoto na mandhari nzuri ya Ziwa Victoria, inafaa zaidi kwa mapumziko ya kifamilia na watalii wanaotafuta sehemu nzuri ya kustarehe. Inapatikana kwa mwendo wa dakika 30 kwa kuendesha gari kutokea jijini Mwanza.  

Kigoma Hilltop. Ikiwa ni kituo cha kuvifikia kwa wepesi vivutio vya kitalii katika ukanda wa Magharibi, hoteli hii ya kisasa imejengwa mbali kidogo na mji, kwenye eneo kubwa la milima linalotazamana na Ziwa Tanganyika. Ukiwa hotelini hapa utafurahia mandhari nzuri ya kuvutia ya Ziwa Tanganyika, lenye sifa ya urefu na kina kirefu Afrika na duniani, kutoka kwenye kila chumba. Shughuli za kitalii zipo lukuki mkoani Kigoma kama vile safari za boti ziwani, kupiga mbizi ziwani, kutalii miji ya kihistoria ya Ujiji na Livingstone pamoja na safari ya siku nzima ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe.   

Kungwe Beach Lodge. Ni hoteli ya kifahari yenye ufukwe wa kuvutia inayopatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale. Ukiachana na mazingira tulivu na vyakula mbalimbali, mgeni anaweza kufurahia shughuli kama vile ziara ya kwenda kuwaona sokwe, kutazama ndege wa mwituni, kutalii mbugani, safari ya boti ziwani, uvuvi, pamoja na matembezi binafsi kwenye fukwe safi pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Maeneo ya kutembelea ni mengi na yanafikika kwa urahisi zaidi na gharama nafuu endapo utaanza kufanya maandalizi mapema. Sikukuu zinakaribia, naamini miongoni mwenu mtakuwa na mapumziko mafupi. Hivyo ni vema kukitumia kipindi hiko kufanya kitu ambacho kitaacha kumbukumbu katika mwaka huu. Unaweza kufahamu mengi zaidi juu ya sehemu hizo kupitia mtandao wa Jumia Travel.

Monday, 12 March 2018

  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiongea na viongozi wa chama cha mapinduzi jimbo hilo walipokutaka mjini mafinga kuzungumzia changamoto za jimbo hilo na nini kifanyike kutatua changamoto hizo
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi amesema kuwa vijiji vyote vya jimbo hilo vitapatiwa umeme wa LEA ambao unafadhiliwa na serikali kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi waliopo vijijini

Chumi amewatoa hofu hiyo wananchi wa jimbo hilo juu ya upatikanaji wa umeme wa LEA wakati alipofanya mkutano na viongozi wa chama cha mapinduzi wa kata zote wa jimbo hilo.

Lakini mbunge huyo alitoa dira ya muelekeo wa jimbo hilo kimaendeleo kwa kuwakumbusha wapi walikotoka na wapi wanaendelea

Friday, 9 March 2018




Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini na ne ya Tanzania kupitia programu yake ya Uhakika wa Maji, imetangaza kuongezwa muda wa uwasilishwaji wa machapisho na programu za redio na runinga kutoka kwa waandishi na vyombo vya habari ili kuwania tuzo za uandishi wa habari za maji.


Tuzo hizi, zilizinduliwa  na Shahidi wa Maji pamoja na washirika wake kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka 2017, na kupewa jina la ‘Tuzo za Habari za Maji. Ili kushiriki katika tuzo hizi, waandishi watapaswa kuwasilisha kazi zao walizochapisha au walizorusha katika vyombo mbalimbali vya habari zinazohusu masuala mtambuka ya maji kama vile; usimamizi na utawala wa rasilimali maji, ukame, mafuriko, usambazaji maji, uchafuzi wa mito na vyanzo vya maji na kadhalika.


Vyombo vya habari pamoja na waandishi watakaoshinda tuzo hizi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, vifaa vya kuboresha ufanisi wa kazi kama vile kamera na kompyuta mpakato, kombe la tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki, hii ikiwa na lengo la kuboresha uwajibikaji miongoni wa wadau wa sekta ya habari katika kuchapa na kusambaza habari zihusuzo maji ili kuleta mabadiliko chanya, endelevu na ya kudumu katika sekta ya maji na kuleta hali ya usalama na uhakika wa maji kwa watanzania wote.


Pia, makala/kazi a za washindi   zitapata fursa ya kurushwa kwenye tovuti zetu na kusambazwa katika vyomba mbalimbali vya habari na mitandao ya kimataifa kama vile: BBC, UK Guardian, Circle of Blue and Ooska News ambayo ni nafasi na fursa ya kipekee kwa waandishi na vyombo vya habari kusomwa zaidi na kutambuliwa kwa mchango wao katika kusaidia kuboresha sekta ya maji nchini.
Tuzo hizi zimeandaliwa mahsusi kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinatoa taarifa za masuala ya maji, kuchochea mabadiliko chanya katika uwajibikaji wa wadau wa sekta ya maji.  Shahidi wa Maji na washirika wake imejikita katika kufanya kazi kubadilisha namna ambavyo rasilimali maji inasimamiwa kwa manufaa ya wananchi wote, mazingira na uchumi wa nchi. Aidha, ili kufanikisha hayo shirika hilo na washirika wake wanafanya kazi kwa namna mbalimbali kama vile; Kusaidia jamii zenye uhitaji kuweza kutambua haki na wajibu walionao katika kuwezesha utekelezaji wa sheria zilizopo na kuwezesha jamii kufuatilia utatuzi wa matatizo ya usalama wa maji katika maeneo yao kwa watoa huduma ikiwemo serikali na sekta binafsi.


Mwisho wa uwasilishaji wa kazi za waandishi na vyombo vya habari umetajwa kuwa tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2018. Kufahamu zaidi kuhusu namna ya ushiriki na kupakua chapisho la maelekezo, vigezo na masharti tafadhali tembelea http://www.shahidiwamaji.org au tuma baruapepe kwenda kennedymmari@shahidiwamaji.org

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe ishara ya uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018

Na Mathias Canal, Chato-Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Maguguli Leo 9 Machi 2018 amezindua jengo jipya la Benki ya CRDB Tawi la Chato Mkoani Geita.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe Dkt. Magufuli amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo utarahisisha huduma za uhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wa samaki Wilayani Chato sambamba na wananchi ambao kwa kiasi kikubwa katika msimu wa Kilimo wamenilima Pamba kwa wingi.

Ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuzifungia baadhi ya Benki nchini na kuzipa onyo zingine ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwa mazoea na kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za uendeshaji.

Alisema ni bora kuwa na Benki chache nchini ambazo zinaweza kuwahudumia wananchi wengi hususani masikini kama ilivyo CRDB ambayo imewafikia kwa kiasi kikubwa wananchi vijijini hivyo kuendelea kuzifungia Benki zote ambazo zimeshindwa kuendesha vyema shughuli zake na kusalia kufanya huduma Jijini Dar es salaam pekee.

Rais Magufuli ameiomba benki ya CRDB kupunguza riba ya mikopo kwani ni asilimia 16 pekee ya watanzania ndio wanaohudumiwa kwenye Benki nchini hivyo ili wananchi wote waweze kukopa na kuweka mitaji yao midogo kwa ajili ya faida yao ya Sasa na badae ni lazima kuwa na riba rafiki kwa wananchi.

JPM ameipongeza Benki hiyo kwa kuajiri wafanyakazi wapatao 3200 tangu ilipoanza rasmi nchini mwaka 1972 wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeielewa dhana halisi ya kuwasaidia wananchi vijijini kutokana na usumbufu mkubwa wanaoupata katika huduma za kifedha.

Alisema kuwa anayo imani kubwa na Benki ya CRDB kwani naye ni mteja wa benki hiyo hivyo ili kuendeleza mahusiano mema tayari seikali imelipa Deni lote la shilingi Bilioni 16 ambalo ilikuwa inadaiwa na benki hiyo kutokana na mikopo katika miaka ya nyuma.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewahamasisha wananchi kutunza fedha zao benki na kuachana na dhana ya kuhifadhi fedha majumbani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa fedha hizo na maisha yao wenyewe.

Mhe Magufuli amesisitiza watanzania kuwa wazalendo huku akisema kuwa anatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamesalia na jukumu la kuandika katika mitandao na vyombo vya habari mambo ambayo ni kinyume na utendaji wa serikali jambo ambalo ni uchonganishi dhidi ya wananchi na serikali yao.

Aidha, Mhe Rais Magufuli alikataa ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei aliyetaka Benki hiyo kuitwa CRDB JOHN POMBE MAGUFULI-CHATO huku akisema kuwa isalie kuitwa CRDB tawi ka CHATO.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania, Dkt Charles Kimei ametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Benki hiyo huku akielezea namna ambavyo amekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua watanzania kupitia rasilimali zao jambo ambalo litawanufaisha na kuwainua kiuchumi.

Alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kubuni njia nzuri za mikopo huku akisisitiza kuwa Benki hiyo kuendelea kuwasaidia wananchi kupitia SACCOS zao kupata mikopo nafuu ili kujinufaisha kwa kuwa na uchumi imara utakaowawezesha kukuza biashara zao.

Sambamba na hayo pia amekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati la kujenga uwanja wa kisasa wa Mpira wa miguu ambapo kwa niaba ya Benki hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Benki ya CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari amekabidhi Hundi la Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya hatua za mwanzo za kuanza ujenzi wa uwanja huo huku akiahidi Benki hiyo kuwa wadhamini wa timu ya mpira wa miguu ya wilaya ya Chato.

Dhifa ya uzinduzi wa Benki hiyo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Wa Nishati Mhe Medard M.Kalemani (Mb), Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Mkuu Wa Mkoa Wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Naibu Waziri Wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijazi (Mb), Naibu Gavana Wa Benki Kuu Tanzania Dkt Bernard Yohana Kibese, Balozi Wa Denmark nchini Tanzania Mhe Einar Hebogard Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari, Mkurugenzi Mtendaji CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, na Wabunge wa majimbo mbalimbali ikiwemo jimbo la Busanda na Mbogwe.

MWISHO. 

Thursday, 8 March 2018

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanawake wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanaume wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanawake wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia na kukata keki ya pamoja
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kilishwa keki na mmoja wa wafanyakzi wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia 

Na Fredy Mgunda,Iringa.
 
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amewataka wanawake mkoani iringa kujifunza kujitegemea katika maisha kutokana na benk nyingi kutoa mikopo yenye riba ndogo ambayo inawasidia kuwainua kiuchumi.

Akizungumza na wafanyakazi wa benk ya NMB tawi la mkwawa Kabati alisema kuwa benk hiyo imesaidia kuinua maisha ya wanawake kwa kuwawezesha mitaji ya kufanyia biashara mbalimbali.

“Mimi nimeshuhudia mara kwa mara mkiviwezesha vikundi vingi vya wanawake ambavyo mmesaidia kukuza maendeleo ya wanawake wa mkoa wa Iringa na ndio maana wanawake wengi wamekuwa wakitoa ushuhuda mzuri juu ya huduma za nzuri za benk hii” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuwa nguzo ya uchumi kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inataka nchi kuwa ya viwanda hivyo wanawake wasiogope kukopa kwenye benk ya NMB kwa kuwa inamashariti nafuu.

“Tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda hivyo wanawake tunapaswa kushikamana kwenye uchumi wa viwanda kwa kuwa benk ya NMB inasaidia maendeleo ya wanawake kwa kuwawezesha mitaji ya kufania maendeleo” alisema Kabati 

Aidha Kabati amewataka wanawake kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa kuwa benk ya NMB imekuwa ikitoa mikopo ya kufanikisha wajasiliamali kuanzisha viwanda.

“Hata saizi ukitaka wajasiliamali waje kwenye kazi furani utakuta wanawake wamekuja kwa wingi kwa kuwa kwasasa wanawake ndio wanafanya biashara ndogo ndogo hivyo wanawake wanaweza kufanya biashara yoyote” alisema Kabati

Kabati aliwataka wanawake kufanya kazi zaidi ya moja ili kuinua na kujiletea maendeleo na kuondokana na kuwa tegemezi kwa wanaume.

Naye meneja wa benk ya NMB tawi la mkwawa George Mwita alisema kuwa bank hiyo imekuwa ikiwawaezesha wanawake kwa kuwapatie elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mikopo yenye riba ndogo.

“Sisi kama NMB benk tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana na wanawake kwa kuwa tunajua wanauwezo mkubwa wakufanya biashara ndogo ndogo na zile kubwa” alisema Mwita

Mwita aliwataka wanawake kufika kwenye benk ya NMB ili kujua huduma ambazo zinatolewa na benk hiyo ambayo ipo kila mahali kwa ajili ya kukuza uchumi wa wanawake na wanaume kwa kuwa benk hiyo haichagui mtu bali inawawezesha wananchi wote.

Ukija hapa benk ya NMB utapata huduma bora ambayo itakusaidia kuinua uchumi wako na kuleta maendeleo kwa kuwa tunatoa mikopo mbalimbali yenye mashariti nafuu na riba yetu sio kubwa” alisema Mwita

Wednesday, 7 March 2018

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita juu ya umuhimu wa kufuata taratibu na sheria katika uchimbaji, Jana 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza akisisitiza jambo wakati aliokuwa akihutubia wananchi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu (Kulia) wakisikiliza kero za wananchi wakati wa ziara ya kikazi Wilaa ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Geita

Serikali imesema kuwa imedhamiria kuwanufaisha wananchi wake kupitia rasilimali za nchi hususani sekta ya Madini hivyo jukumu la Wachimbaji hao ni kufuata maelekezo ya serikali ikiwemo taratibu na sheria katika uchimbaji.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa rai hiyo Jana 6 Machi 2018 wakati akizungumza na wachimhaji wadogo katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.

Alisema kuwa Serikali tayari imetenga maeneo maalumu kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Geita na maeneo mengi nchini huku akisisitiza kuwa kuna leseni za utafiti na uchimbaji mdogo 20 ambazo zinaisha muda wake 30 Machi mwaka huu katika Wilaya ya Nyang'wale hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kwani serikali inatazama namna ya kuwapatia wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo hayo.

Mhe Biteko alisisitiza hayo wakati akijibu maswali ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara na kuiomba serikali kuwapatia maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji kwani katika kipindi kirefu wamekuwa wakizuiwa kuchimba katika maeneo mbalimbali ambayo yana leseni za uchimbaji.

Alisema kuwa serikali itatoa leseni kwa ajili ya maeneo ya uchimbaji lakini haitatoa leseni hizo kwa mtu mmoja mmoja badala yake amewasihi wachimbaji hao kuanzisha vikundi ili kupatiwa leseni hizo.

Mhe Biteko pia alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wwale Mkoani Geita Mhe Hamim Gwiyama kuitisha kikao ndani ya wiki moja kwa kuwaalika wananchi wote wenyewe vikundi ili kuwaelekeza namna bora ya kufanya kazi za uchimbaji kwa kufuata taratibu na sheria.

Aidha, amewataka Wachimbaji hao Mara baada ya kupewa maeneo ya uchimbaji kuwa waaminifu kwa serikali yao kwa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kuboresha huduma za maendeleo ikiwemo sekta ya Afya, elimu na miundombinu.

MWISHO.

Tuesday, 6 March 2018

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.
Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.
Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.
Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia sheria za nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa inapojitokeza.
Akisitikishwa na mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema kutofahamu undani wa soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa wazi na kufanya biashara kwa kufuata kanuni.
Akizungumzia kuhusu madai ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia amewataka Watanzania kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara itakayowawezesha kupata faida kubwa.
Akiutambulisha Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw. Salum Awadh amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi.
Alisema kwamba wakati umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo duniani za mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika hilo.
Alisema kwamba kutokana na kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye ubia, wananchi wengi wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia wanapambana na vikwazo vingine.
Alisema kwa kuwa na kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji inayomilikiwa na wananchi wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo na uimara wa viwanda na kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa mitaji ni tofauti na kwenda benki.
Tanzania kwa sasa ina zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo mbalimbali yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.
Alisema mazingira ya sasa yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia upatikanaji wa mitaji nje ya mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia wa mitaji kutasaidia kuziba pengo lililopo.
Kwa sasa Tanzania kwa rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia ya dola bilioni 2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara mbalimbali.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kulia) wakiwasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto aliyesimama), Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kulia) pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward Furaha (kulia).
Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa maelezo kuhusu Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) kabla ya kuelekea kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kulia).
Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa neno la ukaribisho na kutambulisha mtandao huo ambapo amesema ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mtandao huo ilyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Bw. Edward Furaha na Aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Abdullah Mwinyi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na kubadilishana mawazo na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akibadilisha na mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van Dijk-van de Reijt wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Tanzania Venture Capital Network-TVCN katika picha ya pamoja na mdau aliyewezesha kufanyika kwa uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.