Showing posts with label tangazo. Show all posts
Showing posts with label tangazo. Show all posts

Wednesday, 14 March 2018


                       
                                    YUNUS HUSSEIN  {ALIYEPOTEA}

MTOTO  YUNUS HUSSEIN PICHANI JUU MWENYE UMRI WA MIAKA 12 AMEPOTEA  NYUMBANI KWAO TOKEA TAREHE 8 MPAKA SASA HAJAONEKANA.
 HIVYO KWA YEYOTE ATAKAE MUONA MAHALA POPOTE ATOE TAARIFA KWA NAMBA ZIFUATAZO 0655090202/ 0655141464/ 06585000510
 AU ATOE TAARIFA KATIKA KITUO CHOCHOTE KILICHOPO KARIBU YAKE- MTOTO YUNUS ANAISHI MBEZI JUU JIJI DAR ES SALAAM NA RB NO NI MBJ/RB/236/2018.

Tuesday, 13 March 2018

Na Jumia Travel Tanzania


Zimebaki takribani wiki tatu kabla ya sikukuu ya Pasaka kusherehekewa duniani kote, je umeshafahamu utakwenda kupumzika wapi? 

Pasaka ni miongoni mwa sikukuu zinazopendwa na watu wengi kwa sababu husherehekewa kwa takribani wiki moja. Wakati wa sherehe hizi watu huitumia fursa hiyo kwa kufanya mapumziko ya muda mfupi kabla ya kurejea kwenye shughuli zao za kila siku.

Katika kukusaidia sehemu za kwenda kutembelea sikukuu hii, Jumia Travel imekukusanyia hoteli tano za kuvutia zilizopo pembezoni mwa Tanzania ambazo unaweza kwenda kupumzika kipindi cha likizo hii fupi.

Lupita Island Lodge. Ni hoteli ya kuvutia na tulivu inayopatikana kwenye kisiwa kinachomilikiwa na mtu binafsi ndani ya ziwa Tanganyika. Hoteli hii ina kiwanja binafsi cha ndege na boti ambazo huwachukua wageni kutoka nchi kavu mpaka kisiwani. Hii ni sehemu ambayo unapaswa kwenda kwa ajili ya mapumziko kwa sababu hata namna ya muundo wa vyumba na mazingira yake yamewekwa kumpatia mtu utulivu na usiri akiwa mapumzikoni. Miongoni mwa shughuli za kuvutia ukiwa kisiwani hapa ni pamoja na kutembelea kijiji cha wavuvi, kutalii ziwani kwa kutumia boti na burudani za maonyesho ya kiasili kutoka kwa wanakijiji.  

Katuma Bush Lodge. Ikiwa inapatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi, hoteli hii imejengwa katika mtindo wa kuvutia na kustarehesha kwa kutumia mahema. Eneo hili linatoa wasaa mzuri kwa wateja kutembelea mbuga yenye mandhari nzuri ya uwanda wa Katisunga. Kwa kuongezea, ni sehemu nzuri kwa watalii ambao wangependa kutembelea na kujionea mazingira mapya tofauti na yale waliyokwishayazoea.  

Wag Hill Lodge & Spa. Hoteli ina mazingira tulivu na vifaa vya kisasa, sehemu kwa ajili ya michezo ya watoto na mandhari nzuri ya Ziwa Victoria, inafaa zaidi kwa mapumziko ya kifamilia na watalii wanaotafuta sehemu nzuri ya kustarehe. Inapatikana kwa mwendo wa dakika 30 kwa kuendesha gari kutokea jijini Mwanza.  

Kigoma Hilltop. Ikiwa ni kituo cha kuvifikia kwa wepesi vivutio vya kitalii katika ukanda wa Magharibi, hoteli hii ya kisasa imejengwa mbali kidogo na mji, kwenye eneo kubwa la milima linalotazamana na Ziwa Tanganyika. Ukiwa hotelini hapa utafurahia mandhari nzuri ya kuvutia ya Ziwa Tanganyika, lenye sifa ya urefu na kina kirefu Afrika na duniani, kutoka kwenye kila chumba. Shughuli za kitalii zipo lukuki mkoani Kigoma kama vile safari za boti ziwani, kupiga mbizi ziwani, kutalii miji ya kihistoria ya Ujiji na Livingstone pamoja na safari ya siku nzima ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe.   

Kungwe Beach Lodge. Ni hoteli ya kifahari yenye ufukwe wa kuvutia inayopatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale. Ukiachana na mazingira tulivu na vyakula mbalimbali, mgeni anaweza kufurahia shughuli kama vile ziara ya kwenda kuwaona sokwe, kutazama ndege wa mwituni, kutalii mbugani, safari ya boti ziwani, uvuvi, pamoja na matembezi binafsi kwenye fukwe safi pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Maeneo ya kutembelea ni mengi na yanafikika kwa urahisi zaidi na gharama nafuu endapo utaanza kufanya maandalizi mapema. Sikukuu zinakaribia, naamini miongoni mwenu mtakuwa na mapumziko mafupi. Hivyo ni vema kukitumia kipindi hiko kufanya kitu ambacho kitaacha kumbukumbu katika mwaka huu. Unaweza kufahamu mengi zaidi juu ya sehemu hizo kupitia mtandao wa Jumia Travel.

Friday, 29 July 2016

Zanzibar Diaspora Association inapenda kuwaalika kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Siku ya Jumamosi July 30th -
MAHALI: 42 Charles St Boston
MA 02122.
MDA: Kuanzia 5:pm mpaka 7:pm
Mgeni rasmi ni Katibu mkuu wa CUF. 
Maalim Seif Shariff Hamad
Nyote mnakaribishwa

Thursday, 28 July 2016

Al-Maktoum College of Engineering and Technology (AMCET) Mbezi beach, inatangaza nafasi za masomo katika kozi za umeme,  electronics na computer ngazi ya cheti na diploma.  Mwombaji wa cheti awe ana  'D' 4 form 4, ufaulu wa Math lazima.

Diploma awe na 'D'1 na 'S'1 form 6. Ada cheti 650,000, diploma 750,000. Maombi kupitia NACTE www.nacte.go.tz.

Mwisho 05/08/2016. Hostel zipo,  na program za jioni kwa waajiriwa zipo. 0713220304/0752592504

Thursday, 26 May 2016

Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Doto Mwaibale

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza  ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi  yanayotarajiwa kufanyika katika  Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat,  alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika maonesho hayo.

Alisema Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya  na yatatoa mwanya wa kuyaelewa  masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.

 “Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la  kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara  kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika  kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha  kuwa Tanzania ni ya kwanza  katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.

“Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji  kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.

Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO  inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji  walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.

Alieleza kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza, hii inatoa  fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.

Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza  ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara. 

“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao,  umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.

“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya  usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika  kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya  biashara ya kimataifa  pamoja na 
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
 Alisema kwamba maonesho mengine  ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.



Friday, 19 February 2016