Gari la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadick likiwasili Dampo kuu la taka la Pugu Kinyamwezi, lililopo maeneo ya
Gongo la Mboto jijini Dar alipofanya ziara ya ghafla kwenye dampo
hilo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na.
Damas Makangale, MOblog
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ametoa agizo mara moja kwa
uongozi wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha
miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka
katika dampo hilo. MOblog inaripoti
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya na jiji hivi
karibuni baada ya kufanya ziara ya ghafla katika maeneo kadhaa ya jiji la
Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa amesema tatizo la miundombinu ya barabara
kuelekea katika Dampo la Pugu Kinyamwezi linasababisha foleni kwa malori
ya kusomba taka katika jiji la Dar.
"mara
ya mwisho wakati nakuja hapa kukagua hili dampo kulikuwa na taa na kazi
ilikuwa inafanyika usiku na mchana sasa kumetokea nini," alihoji Mkuu huyo
wa Mkoa
Sadick
aliagiza kwa viongozi wa jiji kushughulikia haraka tatizo la miundombinu ya
barabara kuelekea Dampo ili kuongeza tija katika kazi ya kumwaga na kusomba
taka katika jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka
halmashauri ya jiji, Bi. Enezael Ayo (kushoto) akifafanua jinsi magari ya
taka yanavyomwaga taka katika dampo kuu taka la Pugu Kinyamwezi jijini Dar
wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.
Alisisitiza kwamba utaratibu mbovu wa umwagaji taka na
miundombinu mibovu katika Dampo la Pugu Kinyamwezi vinasababisha mrundikano
wa taka katika manispaa zote za Temeke, Ilala na
Kinondoni.
Amesema kwamba ni muhimu kwa viongozi wa jiji kupata
nguvu kazi ya kutosha ili kuwe na watu watakaosimamia umwagaji wa taka
wakati wa usiku ili kudhibiti madereva wakorofi wanaomwaga taka ovyo bila
kuzingatia taratibu.
Sadick
aliongeza kuwa watendaji wa jiji ni lazima wawe na utaratibu wa kutoa
mafuta kwa wakati kwenye magari ya kusomba (Bull Dozer) na vitendea kazi
vingine.
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa agizo
mara moja kwa uongozi wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi,
kurekebisha miundombinu ya barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji
wa taka katika dampo hilo. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Ndg. Raymond Mushi(mwenye suti nyeusi).
Wakati
akitembelea maeneo kadhaa kati kati ya jiji kuanzia soko la Kisutu na mitaa
ya Libya, Mkuu wa Mkoa aliagiza mamlaka zinazohusika kushughulikia haraka
tatizo la maji machafu kupunguza harufu na kuzuia magonjwa ya
mlipuko.
"nawaagiza mkae pamoja na mje na mpango mkakati
utakaowezesha kumaliza tatizo la maji machafu yanayotoka katika mitaro na
mifereji ya maji machafu katika ya jiji," aliongeza
Wakati
huo huo, wadau kadhaa wa usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam
wameomba serikali kutoa kipaumbele kwa Dampo la Pugu Kinyamwezi na
kulitengea bajeti ya kutosha ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima Enterprises, Bw. Robert
Ngeleshi akizungumzia changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka
katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara
hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick aliyeambata na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ndg, Raymond Mushi wakiondoka eneo la tukio mara
baada ya kuhitimisha zoezi la kukagua miundo mbinu ya Dampo la taka la Pugu
Kinyamwezi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Minael
Mshanga.








0 comments