KATIBU Mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Kaduguda, amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mtaa wa Rufu, Mbande jijini Dar es Salaam na sasa ameahidi kupeleka uzoefu wake katika michezo mahali hapo ili kuleta maendeleo.
Kaduguda ambaye pia aliwahi kuwa Katibu wa Kamati ya Muda iliyoongoza Chama cha Soka Tanzania (FAT) kabla akijabadilishwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mbali na kutwaa nafasi hiyo ya ujumbe, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la Mbande.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kaduguda alisema: “Nimeamua kujikita kwenye siasa kwa sababu ya kuboresha maisha ya watu wa Rufu nikishirikiana na wenzangu na katika maboresho hayo nataka kuitumia uzoefu wangu katika michezo kuwanufaisha watu wa Mtaa wa Rufu.”
Awali alikuwa Mjumbe wa Shina 67 Mtaa wa Rufu. Amechaguliwa pamoja na Mwenyekiti, Idd Kapambala.



0 comments