Thursday, 18 December 2014

UJUMBE WA LEO: KUWATENDEA WEMA WAZAZI

Mmoja wa watu wema alifiwa na mama yake. Wakati mama yake anapelekwa kuzikwa. Alikua akilia sana tena sana. Akaulizwa yule mtu mbona unalia sana kiasi hicho. Akajibu maneno mazito kwa mwenye kutafakari “ Kwa hakika nina huzuni sana ya kufiwa na mama yangu, lakini kinachoniliza zaidi ni kuwa Allah ameufunga mmoja wa mlango wangu wa peponi”

Subhana Allah! Analizwa kwa sababu anajua hatopata tena kumfanyia wema mama yake. Hatopata tena kumtumikia mama yake. Hatopata tena kumfurahisha mama yake. Na haya yote ni njia ya mja kuelekea Jannah.

Leo mtu ana mzee wake anamkimbia. Anatumwa na mzee wake wala sio katika shari yeye anakimbia au anachukia. Tambua unakimbia peponi na kuelekea motoni. Ikiwa una mzee wako yuko hai tambua ni moja katika milango ya peponi.

Mtumikie,mfurahishe,mlishe kwa mkono wako atakufurahisha aliyetuumba ambae ni Allah(subhanahu wataala). Usimtii tu katika kumuasi Allah.

Ama yule mzee wake aliyefariki usimsahau katika dua zako kila siku. “Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.” [Suratul Israa:23].

0 comments