Wednesday, 25 February 2015

BUNGE LA AUSTRIA KUPITISHA UZUIWAJI WA MISAADA KWA WAISLAMU

Bunge la Austria lajiandaa kujadili mswada utakaowanyima waislamu uhuru wa kupokea msaada wa kimataifa

Bunge la Austria linajiandaa kujadili mabadiliko yenye utata kuhusiana na sheria dhidi ya Uislamu.

Sheria hiyo mpya itazuia ufadhili wa kifedha kutoka mataifa ya nje katika ujenzi wa misikiti .

Ufufuaji wa sheria hiyo iliyodumu nchini humo kwa kipindi cha karne moja iliyopita utawaruhusu wakristu na wayahudi kupata ufadhili kutoka mataifa ya kigeni ilahali inawanyima waislamu uhuru wa kupokea msaada kutoka ughaibuni.
Wakristu na wayahudi wataruhusiwa kupokea misaada iwapo sheria hiyo itapitishwa lakini Waislamu na Masheikh hawatoruhusiwa
Kwa mujibu wa waziri wa mtagusano na umoja wa taifa, Sebastian Kurz, sheria hiyo inalenga kuilinda mtagusano wa taifa japo viongozi wa Kiislamu wamepinga vikali mswada huo wakisema utawabagua.

Bwana Kurz amesema wazo la kubadilisha sheria hiyo limetokana na mashambulizi yaliyotokea huko Ufaransa na Denmark.

Aidha mapumziko ya siku zao takatifu kutoka kazini bila ya kupewa adhabu na pia kupata muongozo wa kiroho katika taasisi kadha za serikali kama vile magereza na hospitalini.


CHANZO: BBC SWAHILI

0 comments