Thursday, 26 February 2015

NAMPENDA HUYU, SIMPENDI YULE

Akiugua tunayempenda tunasema ni mtihani,,,,,,
Na akiugua tusiyempenda tunasema ni adhabu...!

Na anapopata msiba tunayempenda tunasema kwasababu ni mwema,,,,,,,,,
Na tusiyempenda akipata msiba tunasema kwasababu amedhulumu watu....!

Jihadhari na kugawa kadari za Allah kwa matamanio yako..!!

Sote tumebeba aibu na lau si nguo kutoka kwa Allah inayoitwa 'sitara' shingo zetu zingeinama kwa kuona haya... basi usiaibishe watu na aibu unayo wewe.....!

YA ALLAH swt TUMUACHIE ALLAH swt

Mtoto alimuomba mamake amueleze kwa ufupi ujuzi wake na hikma alopata maishani, mamake akamwambia: "utaweza kusikiliza?"
Akajibu: ndio......
Mama akasema:

mwanangu: jichunge na kuzungumzia watu au mambo hadi uhakikishe ukweli wake, na akikujia mtu na habari yoyote hakikisha kabla kukimbilia......!

na jihadhari na uvumi
Usiamini kila linalosemwa, wala nusu ya unayoyaona, na Allah akikuonja kwa adui pambana naye kwa kumfanyia hisani... sukuma uovu wake kwa lililo jema, nakuapia kwa Allah uadui utageuka mapenzi...

ukitaka kumjua undani rafiki; safiri naye!
Safarini mtu hudhihirika uhakika wa undani wake....

watu wakikuhujuma nawe uko kwenye haki furahia; kwasababu ni kama wanasema wewe umefaulu na unaathiri, kwani mbwa aliyekufa hapigwi teke, na haupurwi ila mti unaozaa matunda....!!

mwanangu: ukitaka kuchagua mtu... mtazame kwa jicho la nyuki na usitazame watu kwa jicho la nzi kuangalia ubaya tu ulipo!

Lala mapema mwanangu kwani baraka ya rizki ni asubuhi, nakuhofia uikose riziki ya Allah Alrahman kwa kuwa unakesha....

na nitakuhadithia kisa cha mbuzi na mbwa mwitu ili usimuamini anayefanya hila. Na mtu akikuamini, basi chunga tena chunga usimkhini.....!

nitakupeleka kwenye nyumba ya simba nikuoneshe kuwa simba hakuwa mfalme wa msitu kwa kuwa ananguruma ! Lakini ni kwasababu yeye ana ezi ya nafsi, hali windo la mwenzake hata akawa na njaa sana, basi usiibe juhudi ya mwenzako ukawa dhalimu....!!

nitakupeleka kwa kinyonga, ili uone mwenyewe hila zake.! Anajigeuza rangi kwa rangi ya sehemu aliyo, ujue katika watu pia kuna mfano wake.....!!

jizoeshe kushukuru mwanangu.......
Mshukuru Allah inatosha kuwa wewe ni muislamu, inatosha kuwa unatembea, unasikia, unaona,,,,,,,,,,, mshukuru Allah na uwashukuru watu.. Allah anawazidishia wenye shukrani.. na watu wanapenda wakimpa mtu ashukuru.

Sifa njema kubwa katika maisha ni UKWELI.... na jua kwamba uongo hata ukiokoa ni muovu kabisa katika sifa mbovu...

mwanangu.... jiwekee badala ya kila kitu, jitayarishe kwa jambo lolote, ili usidhalilike na kudharaulika.
Na ufaidike na fursa yoyote unayoipata sasa, huenda usiipate tena.

usilalamike wala usijidhalilishe !! Nataka uwe mwenye hisia chanya uyakabili maisha, wakimbie wanaokata tamaa na wenye hisia hasi... na jihadhari kukaa na mtu anayepiga bao...!!

usifurahie msiba wa mwenzako, na jihadhari na kumfanyia stihzai mtu kwa umbo lake, kwani hakuna aliyejiumba.! Na katika kufanya stihzai unakuwa unamfanyie aliye umba.

kwa mafunzo na faida.... matatu:

-na vitatu hutapumzika hadi vikuepuke:
Wasiwasi, deni, na rafiki muovu.

-na watatu jiepushe na kuandamana nao:
Aso na akili, aso jali, aso na utu.

-na watatu usiwafanye marafiki:
Hasidi, na mwenye kijicho, na mwenye kukasirisha wazazi.

-na watatu usivunje rai zao:
Mwenye kuhifadhi sala yake, na mkarimu, na mwenye kuridhisha wazazi.



Imenukuliwa toka katika mtaa wa Radio Imaan

0 comments