Tuesday 19 January 2016

HIKI NDICHO ALICHOPOSTI ZITTO HAPO JANA KUHUSU RUZUKU MASHULENI

Leo nimetembelea baadhi ya Shule za Msingi za Jimbo langu la Kigoma Mjini kukagua utekelezaji wa ruzuku kwa Shule. Manispaa ya Kigoma ina shule za Msingi 46 zenye wanafunzi 42,000. 

Kwa kiwango cha tshs 10,000 kwa kila mwanafunzi Manispaa ilipaswa kuletewa ruzuku tshs 35m kwa mwezi. Hata hivyo Manispaa imepata tshs 25m tu. Pamoja na mapungufu hayo Shule zote nilizotembelea leo zina Kamati za Shule na Mapokeo ya Fedha yamewekwa wazi kwenye mbao za matangazo. 

Hii changamoto mpya ya ‪#‎Uwajibikaji‬

0 comments