Monday, 1 February 2016

GUARDIOLA RASMI KUTUA JIJINI MANCHESTER MWISHONI MWA MSIMU HUU

Taarifa iliyothibitishwa rasmi na klabu ya Manchester City inasema kwamba Pep Guardiola atachukua nafasi ya Manuel Pellegrini kuanzia msimu ujao.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45, atachukua majukumu yake mapema June 30 wakati Pellegrini atakapoondoka Etihad rasmi.

Taarifa kutoka City ilisema kwamba Pellegrini, 62, amekubaliana na uamuzi wa klabu kwa asilimia 100.

“Manchester City inaweza kuthibitisha katika wiki za hivi karibuni ilirudisha mazungumzo na kukamilisha mkataba na Pep Guardiola kuwa kocha mpya wa MCFC kuanzia msimu wa 16/17 na kuendelea. Mkataba ni wa miaka mitatu. Mazungumzo yetu yalikuwa ni muendelezo wa majadiliano ambayo yaliyoishia mnamo 2012.

“Kwa heshima ya Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kuuweka uamuzi huu hadharani ili kupukana na mzigo wa tetesi. Manuel Pellegrini ameusapoti uamuzi kwa kila hali.”

Kocha huyo kutoka Chile aliteuliwa kuwa kocha wa City mnamo mwaka 2013 na kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kombe la ligi msimu uliofuatia.

0 comments