Wednesday, 3 February 2016

TIMU YA SAMATTA YATOLEWA KOMBE LA BELGIUM

Timu anayochezea Mtanzania Mbwana All Samatta Genk FC jana usiku imetolewa katika Kombe la Belgium na Standard Liege katika mchezo wa pili wa nusu fainali wa kombe hilo.

Genk FC wametolewa kwa matokeo ya jumla ya goli 3-1, baada ya jana kutoka sare ya goli 1-1, huku katika mchezo wa awali wakikubali kichapo cha goli 2-0.

Mbwana Samatta hakuhusika katika mchezo huo wa jana, ambapo Genk ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Nikos Karelis katika dakika ya 17 kabla YA Standard Liege kusawazisha katika dakika ya 27 kupitia kwa Adrien Trebel.

Sammata amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea TP Mazembe ya DR Congo ambapo akiwa Mazembe alifanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa Afrika,

0 comments