Thursday 12 May 2016

MeTL YAKANUSHA KUFICHA SUKARI, YAELEZA HALI HALISI

By    
industrial sugar
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa ambayo ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo imeficha sukari tani 2,990 katika Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutembelea ICD na kukuta tani 2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya Mohammed Enterprises jambo ambalo halikuwa na usahihi bali ni mali ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.
Kwaa mujibu wa Murtaza Dewji ambaye ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa sukari hiyo iliingia nchini kwa kufata utaratibu wote kama jinsi inavyotakiwa na anashangazwa kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu sukari hiyo.
“Tulifuata taratibu zote zikiwepo mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.
Aidha ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika nchini tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.
Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali.
Kibali halali cha TFDA hiki hapa chini

0 comments