Monday 2 May 2016

MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

By    
Profesa-Msanjila
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na Modewjiblog)
Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto wa miaka 5-12.
Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.
Alisema dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao katika kazi zinazohusiana na teknolojia.
“Dunia ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,” alisema Keller.
Nae Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues alisema kuwa ni muda muafaka kwa watoto kusaidiwa kupata elimu kwa njia ya kiteknolojia hasa kwa wakati uliopo ambao teknolojia inatumika zaidi katika kurahisisha kazi mbalimbali.
Alisema ni muhimu kwa Tanzania kuanza kutumia mifumo ya teknolojia hasa katika kipindi hiki ambacho nchi ipo katika hatua za kuelekea uchumi wa kati kwani kwa kufanya hivyo itaweza kurahisha kufikiwa malengo kwa muda muafaka ambao umepangwa.
“Ni wakati kwa watoto kupata elimu ya teknolojia, haijalishi hayupo shuleni kwa kipindi hiki teknolojia inatumika zaidi na hii itasaidia wakati huu ambao nchi (Tanzania) inakwenda katika uchumi wa kati,” alisema Bi. Rodrigues.
global-learning-xprize
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya teknolojia lakini inakuwa ni ngumu kufikia malengo hayo yenyewe hivyo ni tumaini lao mradi huo utafanikiwa.
Alisema ni muhimu kwa watoto kupatiwa elimu ya teknolojia kwa dunia ya sasa na serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa pamoja ili mradi huo uweze kufanyika kama jinsi umevyopangwa na Taasisi ya XPRIZE ambao ndiyo waanzilishi wa mradi huo ambao unataraji pia kufanyika nchi mbalimbali duniani.
“Unaposema dunia inakuwa kijiji ina maana unazungumza kuhusu teknolojia kutokana na kusogeza kila jambo karibu na kwa haraka ni ngumu kwa serikali kufanya yenyewe lakini wanapopattikana watu wanaosaidia inakuwa vizuri na pia inasaidia kukuza teknolojia nchini,” alisema Prof. Msanjila.
Nae Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo alisema mradi huo nchini utaanza kwa majaribio katika makundi 200 kutoka mkoa wa Tanga katika wilaya ya Lushoro, Korogwe, Muheza, Pangani, Mkinga, Handeni na Kilindi na mkoa wa Arusha utafanyika katika wilaya ya Ngorongoro ambapo watoto hao watapatiwa simu zilizo na muundo wa tablet na sola za kuchajia na watatumia 'tablet' kwa kusoma, kuandika na kuhesabu na baada ya hapo watakuwa wakichaguliwa kutokana na uwezo binafsi.
Zulmira Rodrigues
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila.
Marina Negroponte, WFP Tanzania
Naibu wa Programu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte (kulia) akizungumzia nafasi ya Shirika lake katika utekelezaji wa mradi wa XPRIZE katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Joel Carnes, Vice President, Operations XPRIZE Foundation - Presentation
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Mafunzo kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akizungumzia malengo ya mradi huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Joel Carnes in Dodoma, Tanzania XPRIZE Launch
Joel Carnes, Vice President, Operations XPRIZE Foundation
Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanyika mjini Dodoma, mwishoni mwa wiki.
Simon Msanjila
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon S. Msanjila (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Zulmira Rodrigues, Head of Office and Representantive to UNESCO Dar es Salaam Office
Kutoka kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila wakifuatilia kwa umakini 'power point presentation' ya jinsi mradi huo utakavyotekelezeka nchini.
Faith Shayo, Education Project Officer, UNESCO Office Dar es Salaam
Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akizungumzia utekelezaji wa mradi huo wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE na wadau watakaoshirikiana nao katika kutekeleza.
Prof. Simon Msanjila
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki, waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta elimu waliohudhuria uzinduzi huo, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Marina Negroponte, WFP Deputy Head of Programme
Naibu wa Programu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte akiandika mambo muhimu kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE.
Faith Shayo
Afisa mradi wa Elimu wa Unesco, Dar es Salaam, Faith Shayo akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller wakati wa uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
IMG_1791
Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu, waandishi wa habari na viongozi kutoka Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hoteli ya Veta, mjini Dodoma.
IMG_1636
Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon S. Msanjila
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila akiagana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller....Kulia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.
Simon S. Msanjila
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Veta mara baada ya kuzindua rasmi mradi huo.
Joel Carnes XPRIZE Launch in Tanzania
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller (katikati) akizungumza na mmoja wa waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Veta mjini Dodoma, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo. Kulia ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.

0 comments