Wednesday, 8 June 2016

HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA KINARA KWA UJANGILI WA TEMBO NCHINI

Mwalimu wa Uchumi na Utalii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  Profesa Wineaster Anderson (kulia), akitoa mada kuhusu uchumi na Utalii katika mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali mjini Morogoro leo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Ibrahim Mussa (kulia), akitoa mada katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Dk. Felician Kilahama (kulia), akitoa mada kuhusu misitu katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Dk.Allan Kijazi, akizungumza jana katika mkutano huo.
Wanahabari Khadija Khalili (kushoto) na Beatrice wakiwa kwenye mkutano huo.
Wahariri, Bakari Kimwaga (kushoto) na Anicetus Mwesa wakifuatilia mkutano huo.

Mwanahabari Lazaro kulia akijiandikisha katika kitabu cha mahudhurio
Wanahabari na wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania (TBN), Joachim Mushi akiwa kazini katika mkutano huo ulihudhuriwa na baadhi ya bloger.
Mhariri wa Nipashe, Jesey Kwayu akiuliza maswali.
Mwanahabari na mpiga picha wa gazeti la mtanzania, Humphrey Shao akiuliza maswali.
'Hapa ni kazi tu' wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Dk. Allain Kijazi amesema Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kinara wa ujangili wa Tembo ukilinganisha na hifanyi nyingine

Dk. Kijazi ameyasema hayo leo mkoani Morogoro katika siku ya pili ya Mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania ulioandaliwa kwa kwa ajili ya wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari.

"Hali hii ya  ujangili inatokana na kuwepo kwa tembo wengi ambapo majangili wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo na kufanya uharifu" alisema Kijazi.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo jitihada kubwa zinafanya kwa kutumia mfumo wa kiokorojia kwa lengo la kuhakikisha udhibiti wa ujangili unafanikiwa na kunusuru ujangili huo unaotishia katika hifanyi hiyo.


Katika hatua nyingine Dk.Kijazi ametoa mwito kwa Serikali kutengeneza miundo mbinu ya barabara na Wawekezaji kujenga mahoteli katika mikoa ya Kusini na Magharibi mwa Tanzania ili kukuza utalii katika maeneo hayo jambo litakalo inua uchumi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa baadhi ya mikoa ya Kusini na Magharibi mbayo inavivutio vya utalii lakini imeshindwa kufanya vizuri katika kuingiza watalii wengi kutokana na miondo mbinu yake ya barabara kutokuwa rafiki.

"Ninaamini waandishi wa habari mkitupigia debe na Serikali ikasikilia kilio hiki na kutengeneza barabara kwa kiwango kizuri na Wawekezaji wakajenga mahoteli hakika itasaidia kuvutia watalii kama ilivyo kwa mikoa ya Kaskazini," alisema.

Alifafanua kuwa mikoa ya Kaskazini ambayo inavivutio imekuwa ikipata watalii wengi kutokana na urahisi wake kufikika kwa maana watalii wanahitaji kutumia muda mfupi kufika mbugani ili atumie muda mrefu kuona wanyama.

Aliongeza kuwa hali hiyo ni tofauti na mikoa ya Kusini na Magharibi ambako mtalii atatumia murefu barabarani na kutumia muda mfupi katika kuangalia wanyama na vivutio vingine jambo ambalo si lengo lake.

Alisema licha miundo mbinu ya barabara za Kusini kutokuwa rafiki kufika katika vivutio, pia hata malazi kwa watalii si ya kuvutia na pengine hakuna kabisa hivyo ni changamoto kwa wawekezaji kuhakikisha wanajenga mahoteli ya kisasa.

Aliweka wazi kuwa ikiwa jambo hilo litafanikiwa kwa kuwa na miundombinu mizuri ya barabara na hoteli zenye viwango hakika watalii katika mikoa ya Kusini wataongezeka.


Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Masoko Tanapa, Ibrahimu Mussa alisema kuwa ili kuinua mapato yanayotokana na utalii nchini malipo ya watalii yanafanyika kwa kadi za kibenki.

"Tumeamua kuondokana na upokeaji wa fedha kwa 'Cash' ili kuondoa upotevu wa mapato jambo litakalosaidia kuinua kiwango cha ukusanyaji wa mapato tofauti na ilivyokuwa awali,"alisema.

Akizungumzia suala baadhi ya watalii kulipia gharama viingilio wakiwa nchini kwao, alisema fedha wanazolipa zinafika Tanzania na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha watalii wanakuwa salama katika mali zao.

Aliongeza kuwa hata mtalii akiumia akiwa hapa nchini akiwa kwenye utalii analipwa bima kupitia nchi yake jambo ambalo linamfanya kuwa salama zaidi.

Pia alisema Tanzania imeshuka katika viwango vya vivutio vya asili ikitoka namba mbili nyuma ya Brazil hadi na namba saba na katika viwango vya jumla inashika nafasi ya 93 kati ya nchi 114 zenye ushindani.

Alifafanua kuwa sababu ya kushuka katika viwango hivyo vya dunia ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uvamizi wa maeneo ya vivutio hivyo na miundo mbinu ya barabara na changamoto zingine zilizopo.


0 comments