Sunday 4 March 2018

BILIONI 1.4 KUBORESHA VITUO VYA AFYA RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kuboresha vituo vitatu vya afya katika wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao,”Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Machi 04, 2018) wakati alipotembelea kata ya Mandawa kwa ajili ya kukagua mradi wa uboreshaji wa kituo cha afya cha kata hiyo.

Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 400 zitakuwa kwa ajili ya kituo cha Mandawa, milioni 500 kituo cha Mbekenyera na milioni 500 Nkowe.

Chanzo : Azam TV

0 comments