Monday 29 April 2013

YADUMU KWA MIAKA MIWILI NA KUTWAA UBINGWA

Na Abdallah H.I Sulayman

Ligi kuu ya Zanzibar Grand malt inaelekea ukingoni wakati KMKM wakiwa teyari wamesha twaa ubingwa wa ligi hiyo na kushuhudia bingwa mtetezi Super Falcon akiwa katika hali mbaya ya kushuka daraja wakichuana na Duma, Mundu na Malindi kusaka nafasi ya kusalia katika ligi hiyo.

Super falcon hayupo katika nafasi nzuri inayoweza kumfanya asalie ligi kuu za Zanzibar Grand malt na kuweza kushiriki ligi hiyo kwa msimu wa tatu toka ipande daraja na kupata tiketi ya kushiriki ligi hiyo.

Super falcon ikiwa na misimu miwili katika ligi kuu ya Zanzibar kuna matukio ya uwanjani na nnje ya uwanja yaliyoisibu timu hiyo na kupelekea kuonekana kama inamda mrefu katika ligi hiyo, ambapo teyari wameshateremka, haya ni matukio yaliyo wasibu Super falcon:

1. BINGWA MTETEZI KUSHUKA DARAJA.

Sahau kuhusu kuchukuwa ubingwa katika msimu wao wa kwanza katika ligi kuu, ila ili la kushuka daraja katika msimu wake wa pili wakitokea kutwa ubingwa wa ligi kuu, huenda ikawa rikodi mpya katika mchezo wa soka ulimwenguni.

2. KUTWAA UBINGWA KATIKA MSIMU WAO WA KWANZA.

Super falcon waliungana na timu nyingi ulimwenguni ambazo zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar katika msimu wake wa kwanza.

3. KUSHINDWA KUSHINDA MICHEZO DHIDI YA TIMU ZA NNJE YA ZANZIBAR.

Super falcon katika misimu yake miwili hawajapata bahati ya kuzifunga timu yoyote inayotoka nnje ya visiwa vya Zanzibar katika michezo ya michuano.

Super falcon wakiwa kama mabingwa walishiriki katika michuano ya kombe ya super8 banc ABC iliyohusisha timu toka visiwani Zanzibar na Tanzania Bara.

4. BINGWA KUSHINDWA KUSHIRIKI KLABU BINGWA AFRIKA.

Super falcon wakiwa kama mabingwa wa visiwani Zanzibar walishindwa kushiriki michuano hiyo kutokana na kukosekana kwa fedha.

5. KUSHIRIKI KAGAME CUP WAKIWA DARAJA LA PILI.

Huenda super falcon watakuwa timu ya kwanza kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati 'Kagame cup' wakiwa wanashiriki ligi daraja la pili kama ukata hauta watatiza.

Muwakilishi wa zanzibar katika michuano ya Kagame huwa ni bingwa wa msimu mmoja nyuma (ina maanisha KMKM wataiwakilisha Zanzibar katika Kagame mwakani) kama taratibu hazito badilika.

0 comments