Friday, 21 June 2013

UNGEAMBULIA NGAPI KATIKA MTIHANI HUU

Na Masanja Mkandamizaji

NIMEIKUTA MAHALI SIJUI NANI KATUNGA HII!



WATOTO WA KISHUA SECONDARY SCHOOL
S.L.P 7677, MASAKI.
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA.


MAELEKEZO
.
i. Jibu maswali yote.
ii. Kila swali linabeba maksi kumi
iii. Zingatia mpangilio wa kazi.
iv. Unaruhusiwa kutumia BLOGS na MAGAZETI YA UDAKU
iv. SWALI LA TISA NI LAZIMA KUJIBU.
MUDA; Masaa matatu.


SECTION A.

1. Kwa kutumia mifano hai, elezea chanzo cha Kim Kadarshian kugombana na Kanye west.

2. Taja tofauti kuu nne kati ya MLIMANI CITY na QUALITY CENTER.

3. Kwa kutumia maeneo ya samakisamaki, Coco beach, Steers, naKunduchi beach resort elezea maanaya neno BATA.

4. Mapenzi hujengwa kati ya msichana na mvulana. Je Vipini masikioni, Kuvaa mlegezo, mwanaume kusuka na kujipaka carolight vinachangia vipi kufanya penzi lichanue? Fafanua!! Tumia mifano hai ya maboyfriend wa watoto wa kishua

5. Kwa kutumia tamthilia za MARA CLARA na zile nyingine za PROMISE na TIMELESS elezea nafasi ya mwanamke katika jamii.



SECTION B

6. Elezea sababu kuu tano za WEMA na Diamond kugombana!! Na kisha elezea mapinduzi yaliyofanywa na Jokate Mwegelo. Na je kwa nini hawakudumu

7. Inasemekana kuwa Chipsi mayai ni mojawapo ya chakula kinachowachanganya wasichana wengi na mwisho kujikuta wametoapenzi. Kwa kutumia maeneo ya Masaki na Mikocheni elezea Baga na Pizza zinavyosababisha tatizo hili.

8. Kwa kuwatumia wasanii wa Bongofleva kama Diamond na wa mtoni kama Chriss Brown elezea maana ya neno SWAGA.

9. Watoto wengi wa kishua hukimbilia kutafuta mademu wa uswazi wakidai kuwa wasichana wa geti kali hawajui lolote kitandani. Elezea kiufasaha ukitumia mifano hai kwanini wasichana wa kishua ni bomu kitandani.

10. Kwa kutumia mifano hai ya PLAYSTATION elezea ni ipi ngumu sana kucheza kati ya PS 2 na PS 3…..


NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!!!



0 comments