Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania umesema hauna
imani na tume iliyoundwa na jeshi la polisi nchini humo kwaajili ya
kuchunguza tukio la kupigwa risasi kiongozi wa kidini Sheikh Ponda Issa
Ponda. Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Baruan Muhuza Mratibu wa mtandao
huo Onesmo Ole Ngurumwa amewaambia waandishi wa habari mjini Dar es
Salaam leo kuwa jeshi hilo halina haki ya kujiundia tume ikiwa lenyewe
ndiyo linatuhumiwa kumpiga risasi sheikh huyo. Ngurumwa amesema kuwa
inasikitisha kuona vyombo vya dolavinaendelea
na uvunjajiwa sheria kwa kutumia nguvu inayokiuka haki za msingi za binadamu.
Chanzo: BBC
0 comments