Thursday 1 August 2013

POLISI ZANZIBAR WAMSAKA PONDA

By    
POLISI Zanzibar inamsaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, kwa tuhuma za kuendesha mihadhara ya kidini katika misikiti kisiwani hapa, yenye kuashiria uvunjifu wa amani.

Ponda anatafutwa kwa tuhuma hizo, wakati akiwa katika kifungo cha nje cha miezi 12, alichohukumiwa Mei 10, katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh milioni 59.6, uchochezi na kuingia kwa jinai katika ardhi inayomilikiwa na kampuni ya Agritanza Limited kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.

chanzo: http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/14726-ponda-asakwa-na-polisi-zanzibar

0 comments