Friday, 2 August 2013

PONDA: HUU NI UTMWA WA SERIKALI KWA RAIA WAKE

By    
Na Abdallah Khamis, Tanzania Daima

SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kuliomba Jeshi la Polisi limkamate Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, akidaiwa kuchochea uasi dhidi ya serikali misikitini, kiongozi huyo ameibuka na kuitaka serikali ijielekeze kushughulikia matatizo ya wananchi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ponda alisema kuwa viongozi wa CCM wamekosa upeo katika kuielekeza serikali yao ishughulikie matatizo ya wananachi na badala yake wanatumia nguvu kubwa kuwadhibiti wale wanaohoji utendaji wa serikali hiyo.
Ponda alifafanua kuwa njia nzuri ya kudhibiti mihemko ya wanaohoji utendaji wa serikali ni kwa viongozi kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi.
Alipotakiwa kufafanua tuhuma za CCM kuwa anachochea udini na uasi dhidi ya serikali misikitini wakati akiwa bado anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja, Ponda alisema kuwa jukumu la viongozi wa dini ni pamoja na kuzungumzia hali ya nchi pasipo kujali kama ipo katika hali nzuri au mbaya.
“Niliyoyasema huko Zanzibar ni sawa, wananchi wanapaswa wasikilizwe na hawa CCM wasikimbilie polisi tu bali watekeleze wajibu wao…nimezungumzia suala la viongozi wa Jumuiya ya Uamsho kunyimwa dhamana wakati kesi inayowakabili ina dhamana sasa kama huo ni uchochezi watuambie,” alisema.
Ponda aliongeza kuwa kinachofanyika ni serikali kuzungusha shauri la watuhumiwa hao kufika mahakamani ili wasipewe dhamana hatua aliyodai ni ukiukwaji wa haki za msingi za watuhumiwa.
Alisema moja ya haki za msingi za mtu aliyekamatwa na vyombo vya dola ni pamoja na kupelekwa katika vyombo vinavyotafsiri sheria ili mtuhumiwa apate fursa ya kusikilizwa huku akibainisha kuwa hilo halijafanyika kwa zaidi ya miezi tisa sasa

0 comments