Radio Imani FM iliyofungiwa kwa miezi 6 hapo february 28 inataraji kurejea hewani hapo agosti 28 mwaqka huu ikiwa ni siku tatu kutoka sasa.
Radio Imani yenye masafa ya 104.5 jijni Dar es salaam yenye ofisi zake mjini Morogoro ilifungiwa a TCRA kwa kuhusishwa kuhamasisha waislamu kuto shiriki katika zoezi la sensa lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana na kusikika viongozi mbalimbali wa serikali wakisema zoezi lilifanikiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja ya watangazaji wa kituo hicho cha redio kinacho rusha matangazo yao yenye maadili ya dini ya kiislamu amesema kuwa kwa sasa wako katika maandalizi ya kurejea hewani, huku akiwaomba waumini waiombee dua ili ifanikiwa kurejea vyema hapo agosti 28 mwaka huu.
Radio Iman FM inamiilikiwa na taasisi ya Islamic Foundation yenye kituo cha television kinachoenda kwa jina la TV Imani vilevile ni wamiliki wa shule ya kiislam ya Daarul-Arqam yenye maskani yake mkoani Morogoro.
MTANDAO HUU PAMOJA NA ABOODMSUNI NETWORK INAITIKIA UREJEO MWEMA WA RADIO IMANI HAPO AGOSTI 28 MWAKA HUU. IINDELEE KUTUTOA KE=WENYE GIZA NA KUTUPELEKA KWENYE NURU.
0 comments