Kutoka kwa MARAFIKI WA REDIO IMAAN
Jina: Mfumo Kristo
Mada: UHURU NA UCHOCHEZI....
Amani iwe nanyi, si jambo la ajabu kusikia mtu kashitakiwa kwa makosa
ya jinai kwa sababu ya kuchapisha au kutamka maneno au maoni ya kawaida,
lakini yanaweza kugeuzwa kwa ufundi wa kisiasa kuwa “uchochezi”, kwa
sababu tu ya kutowafurahisha
baadhi ya wenye madaraka. Uhuru wa kujieleza nchini umedhibitiwa kwa
sheria mbili ambapo unapofikia kiwango fulani huitwa “uchochezi”
(sedition).
Kwa kuanzia, “uchochezi” ni kosa la jinai chini ya Sheria ya
Makosa ya Jinai (Penal Code) kifungu cha 50 na 55; pili “uchochezi” ni
kosa chini ya kifungu 55 cha Sheria ya Magazeti, Namba 3 ya mwaka 1976.
Wakati sheria hizi mbili zinadhibiti uhuru wa kujieleza, kinyume cha
sheria hizo, Katiba ya nchi inatoa uhuru huo bila kikomo, chini ya Ibara
ya 18, kama nilivyoinukuu mwanzo.
Kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, je,
si kweli kwamba yale yanayoitwa “makosa ya uchochezi” si uchochezi bali
ndio uhuru wenyewe wa kujieleza na wa kutoa maoni yoyote? Je, huko si
kuingilia uhuru wa mawasiliano wa mtu? Ni nani mwenye haki ya kuamua
uhalali wa maoni (yoyote) na aina ya uhuru wa mawazo ya mtu katika
kutekeleza haki hiyo ya kikatiba?
Je, ni halali kwa mtu kushitakiwa
chini ya sheria za makosa ya jinai? Ni kiwango gani cha uhuru
kinachovumilika ili usiitwe “uchochezi”?
0 comments