Sisi, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay – atul Ulamaa),
tumepokea kwa masikitiko makubwa habari za kushambuliwa na kujeruhiwa
kwa silaha za moto, Sheikh Ponda Isa Ponda, huko Morogoro, Jumamosi
Agosti 10, 2013.
Hay-atul Ulamaa, imesitushwa na tukio hili linalo uma na linaloumiza na
kuleta mshtuko na fazaa katika jamii kama ilivyoshtushwa na matukio
mengine kama hili hapa nchini. Hili ni tukio ambalo linaashiria kuwa
walio litenda hawaitakii mema na amani nchi yetu.
0 comments