1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA
KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI
MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.
2.
KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU
WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA
AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA
JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA
SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA
UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA
UVUNJIVU WA AMANI.
3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4.
KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA
KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO
KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA
MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5.
KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI
JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU
IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
0 comments