Na Grace Macha, Arusha : TANZANIA DAIMA
MATUKIO ya kumwagiwa tindikali yanazidi kushika kasi ambapo mfanyabiashara, Japhet Minja (30) mkazi wa Sakina, amemwagiwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni tindikali usoni na watu wasiojulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi saa tatu asubuhi maeneo ya Shamsi ambako mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Selian huku macho yake yakiwa yamepoteza uwezo wa kuona.
Akizungumza kwa tabu, Minja ambaye alitolewa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU) jana mchana, alisema kuwa anasikia maumivu makali kwenye macho na ngozi ya uso.
Alisema kuwa Oktoba 8 mwaka huu, wakati akitoka nyumbani kwake maeneo ya Sakina Banda la Maziwa alisimamishwa kwa kupigiwa honi na watu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Vitz ambayo hakumbuki namba zake za usajili.
Minja alisema kuwa alisimama na kuwasikiliza watu wawili waliokuwa kwenye gari hilo ambao walimweleza kuwa walikuwa wanampigia simu kwa namba alizobandika ubavuni mwa gari lake, lakini hawampati, wanahitaji kuwekewa madirisha ya aluminum kwenye nyumba yao na walimpa vipimo.
Alisema kuwa aliwaambia ni vema akafika kwenye eneo husika, lakini walimsisitiza atumie vipimo walivyokuwa navyo, na aliwapigia mahesabu ikaonekana inahitajila zaidi ya sh milioni 4.4.
Kwa mujibu wa Minja, wateja hao walimpa kiasi cha sh milioni tatu kama malipo ya awali, kiasi kingine wangempa akimaliza kazi na kwamba alitaka kuzihesabu fedha hizo, lakini wakamwambia hazina shida akahesabie ofisini kwake, hivyo alizihifadhi ndani ya gari.
“Tuliondoka tukiwa tumeongozana, kufika mbele kidogo tukakuta gari nyingine aina ya Vitz likiwa liimeegeshwa kuziba barabara, ndani kulikuwa na watu wanne.
“Nikaona wale watu wawili walionipa fedha wameenda kuzungumza nao, lakini hawakuondoa gari, hivyo na mimi nikasogea na kuwaomba waondoe gari kwani wengine tunawahi kazi,” alisema.
Alisema kuwa watu wale walishuka na kuanza kumpiga kisha mmoja akampulizia kitu kwenye macho, yakaanza kutoa machozi huku wale waliompa fedha wakikimbilia ndani ya gari lake na kuzichukua.
“Niliamua kukimbilia kwenye gari langu na kurudi nyuma kwani bado yale magari yalikuwa yameziba njia. Nilikwenda duka la dawa wakanimwagia maji usoni na spiriti kwenye kidonda cha mkononi nilipong’atwa kisha wakanishauri niende hospitali.
“Niliendesha gari hadi hospitali ya Selian na wakati wakienda kunipatia huduma nilihisi kushindwa kupumua na nikapoteza fahamu na nilipozinduka baadaye nikajikuta ICU,” alisema.
Dk. Godbless Massawe aliyempokea Minja, alikiri kuwa alimwagiwa kitu ambacho hadi sasa hawajaweza kukibaini kwani vipimo vya kubaini tindikali kwa hapa nchini vinapatikana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pekee.

0 comments