POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.
Tukio hilo limetokea katika mlima Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani MTWARA ambapo pia CDs zenye mafunzo mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen akitaja vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda Zelothe alisema, “Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi, Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu, Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150 na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.
0 comments