Sunday, 20 October 2013

NI DALILI ZA KIAMA????

By    
Na:Ukhti Safina Ahmad: MIMI NI MUISLAMU

Watu leo tunashindana kuonyeshana uwezo wa mali katika mambo ya kidunia.

Sherehe zetu,ndoa,kupel
eka watoto sunna n.k
Hatufanyii tena misikitini au nyumbani kiroho na kiutulivu. Tunafanyia katika mahoteli makubwa na migahawa ya kifahari ambako maskini atajiuliza mara mbili kufika (kama ataalikwa).
Ujumbe unaotolewa kwa maharusi siku hizi nao pia mtihani !

Zamani Mzazi alimwambia binti pindi anapo olewa:
"UNATOKA NYUMBA HII NDANI UMEVAA NGUO NYEUPE YA HARUSI, INSHAALLAH UKATOKE KWA MUMEO NDANI YA SANDA NYEUPE"

Wazazi waliusia Uaminifu,Kujitolea na Kumhamasisha binti kuwa na subra katika ndoa.
Siku hizi wazazi wanawapa ushauri binti zao kana kwamba ni marafiki wanaopeana ushauri!
Mzazi anasema 'hujaua yakikushinda rudi'
au 'akikuona wa nini we muone wa kazi gani'
Sub'haanallah...!binti anajazwa kibri na chuki tangu siku ya kwanza!
Bila shaka si jambo gumu kukisia ni aina gani ya ushauri anaopewa muoaji! TUZINDUKE WAISLAM !

0 comments