NA MIMI NI MUISLAMU
Doctor Gary Miller mwalimu wa hesabu na falsafa katika chuo kikuu cha Toronto nchini Canada. Alikuwa ni katika walinganiaji wakubwa wa ukristo.
Siku moja alichukua uamuzi wa kusoma Qur ani yote kwa lengo la kutafuta makosa, ili aweze tumia ujuzi wake huo katika kuwalingania waislamu waweze ingia katika dini yake ya ukristo.
Kwa kuwa Qur ani imeshushwa karne 14 zilizopita, alikuwa akitarajia atakuta usulubu wa kizamani , habari za majangwa na mfano wake.
Lakini alishangazwa na mambo aliyo kutana nayo !!! Bali akagundua ya kwamba kitabu hiki, kimekusanya mambo mengine ambayo huwezi kuyapata katika kitabu chochote duniani.
Alikuwa anatarajia atakuta khabari za baadhi ya matukio yaliyo mtokea mtume –rehema na amani ziwe juu yake- kama vile kufariki kwa mkewe Khadija-radhi za Allah ziwe juu yake- na kufariki kwa watoto zake Lakini habari kama hizo hakuzipata kabisa.
Bali katika mambo ambayo yalimshangaza sana, kukuta katika Qur anikuna sura kamili inaitwa Surat Mariyam.
Akaona ni jinsi gani Mariyamu-alayhaa salaamu- alivyo tukuzwa,huto ona mfano wake katika injili. Na wala hakukuta sura inaitwa Surat Aisha,au surat Fatwima –radhi za Allah ziwe juu yao-.Akakuta nabii Issa{Yesu}-alayhi salaamu-katajwa kwa jina lake mara 25.
Hali ya kuwa mtume Muhamadi-rehema na amani ziwe juu yake,hajatajwa isipokuwa mara 4 tu ! akazidi kushangazwa na kitabu hiki kitukufu.
Akaendelea kusoma Qur ani kwa umakini zaidi, huenda atapata japo kosa moja. Akiendelea na hali yake hiyo, alishangazwa kukutana na aya ya ajabu iliyo mshitua,aya ya 82 katika surati Nisaa{4}.
(Je hawaizingatii Qur ani? Na law ingekuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake ikhitilafu nyingi)
Dr. Gary Miller anasema:Miongoni mwa misingi ya elimu inayojulikana hivi sasa ni kutoa makosa katika chunguzi mbali mbali.
Anasema lakini jambo la ajabu katika Qur ani ni kwamba, inasema haina makosa ,na inawataka waislamu na wasio kuwa waislamu,kutafuta makosa ndani yake na hawato yapata.
Anasema hakuna mtunzi duniani ambaye anaweza tunga kitabu,kisha akathubutu kusema ya kwamba kitabu chake kimetakasika na makosa. Lakini Qur ani ni kinyume chake. Yakwambia haina makosa,na ichunguze huto pata japo kosa moja.
Vile vile katika aya zilizomshangaza sana Docter Gary Miller, ni aya namba 30 ya surat Anbiyaa,isemayo:
(Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikana, kisha Sisi tukazibabandua{tukaziachanisha}?
Na tukajaalia kwa maji kila kitu kuwa hai, Basi je, hawaamini?)
Anasema maudhuu hii ndio niliyo chukulia zawadi ya Nobel katika uchunguzi wangu wa kisayansi mwaka 1973.Ilikuwa ikizungumzia mlipuko mkubwa ulio tokea katika ulimwengu.
Kwani mbingu na ardhi na sayari nyinginezo, zilikuwa zimeshikana ,kisha ukatokea mripuko mkubwa na kuachana.
Tuje upande wa pili wa aya,inayo zungumzia ya kwamba maji ndio chimbuko la uhai.
(Na tukajaalia kwa maji kila kitu kuwa hai).
Anasema jambo hili ni miongoni mwa mambo ya ajabu sana, kwani wataalamu wamethibitisha hivi sasa ya kwamba, chembechembe za uhai,zimejengeka kutokana na Cytoplasm. Cytoplasm ambayo asilimia 80% ni maji.
Vipi kwa mtu huyu aliye ishi miaka 1400 iliyopita aligundua vitu hivi?! ni nani aliye mfundisha???!!! Hapana shaka ,kweli mtu huyu alikuwa akishushiwa wahyi toka kwa Mwenyezi Mungu.
Dr. Gary Miller akaamua kuingia katika uislamu. Na kuanzia hapo akaanza kutoa mihadhara ya kulingania watu kuingia katika uislamu,na kafanya midahalo na wakristo wengi ambayo nae siku zilizo pita alikuwa ni miongoni mwao. Alhamdulillahi juu ya neema ya uislamu.
Dr. Gary Miller sasa hivi jina lake ni Abdu-Ahad Omar. Ni mwandishi wa kitabu maarufu kinachojulikana kama "THE AMAZING QUR'AAN" yaani "QUR'AANI INAYOSHANGAZA".
Allaah ambariki Dr Abdul-Ahad .
***************************************
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: (Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa) Qur ani 17:9
Na anasema: (Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu). Qur ani 3:19
Na anasema: (Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini iliyokuwa safi kabisa, ndilo umbile ambalo Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui) Qur ani 30:30

0 comments