Friday, 28 March 2014

KITAANI: UJUMBE MDOGO KWA MADADA ZETU

By    

VOICE OF ZANZIBAR in Zanzibar


Tunaandika hili si kwa kumuingilia mtu katika maisha yake ila tunaandika hili kwa kupeana kidogo taaluma na kukumbushana madhara ya mambo tunayoyafanya.

Tunazungumzia MKOROGO,kusema kweli dada zetu hampendezi,kuba
li ulivyoumbwa kama umeumbwa mweusi kuna sababu kwanini ukaumbwa rangi hiyo,shukuru kwa rangi uliyoipata,na wengi wenu mmeona baada ya muda wa kutumia mkorogo vijiso vyenu vinaharibika kwa madoa na mabaka meusi,hapa ndio unajua kuwa uzuri umekutumbukia nyongo uso mweupe pamoja na mabaka meusi na miguu myeusi,sura mpya miguu ya zamani,wacheni jambo hili,wanaume hawavutiwi na jambo hili,kuna baadhi ya hata wanaume na wao wameingia kwenye majanga haya,hili ni wazo tu tumeona tuandike kidogo.Wengi wamepata cancer na magonjwa mengi ya ngozi ni bora na wewe uwache

KAMA HII HABARI UNAHISI IMEKUKERA BAADA YA KUISOMA BASI UJUE UNATUMIA MKOROGO

0 comments