Monday, 24 March 2014

MAIMAMU WATATU WAFUNGWA, WENGINE KUMI WAPIGWA FAINI BULGARIA

By    
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj74AlCkeqJz22WGIAWlQWeqBfjtEXt13Aow7riiQFc3oOkmRwcxktxZAp7GBVNNqR6ChHENC5bOtIowcUcizsMbYIWezpbP1GXApS_dn96VZSkfoFX14mslB6kDTncTgQ0POB3U0iX1bjt/s1600/bulgaria.jpg
Maimamu 3 nchini Bulgaria wamefungwa jela miaka 3 na wengine 10 kupigwa faini ya Euro 2500 kwa makosa ya kueneza itikadi na propaganda za matamshi yenye kuzua chuki kwa wananchi.

Imamu Ahmed Musa Ahmed alihukumiwa mwaka mmoja jela na faini ya Euro 2500.

Imam Said Mutlu na Mutfi Abdullah Saleh nao pia walihukumiwa kifungocha mwaka mmoja faini ya Euro 1,500. Aidha mahakama imezuia pesa na kompyuta tatu zilizokutwa nyumbani kwa Mutfi Abdullah.

Maimamu wengine kumi waliobaki walipigwa faini ya Euro 2,500 kila mmoja.

Wanasheria wa Maimamu hao walisema kuwa wanaweza kukata rufaa hukumu hiyo kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu.


CHANZO: AHBAABUR RASUUL

0 comments