Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa
nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza katika viwanja vya
Mazingira Senta mjini Shinyanga kwenye warsha ya siku moja iliyokutanisha
shule 10 za sekondari, vyuo na walimu kutoka katika shule na vyuo hivyo
vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema Umoja wa Mataifa(UN)
unalipa suala la elimu kipaumbele sana kwa wanafunzi hivyo kuwataka
wanafunzi kuwa na malengo katika maisha yao kwa kusoma kwa bidii,kuepuka
vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito wakiwa wanafunzi tena chini ya
umri wa miaka 18.
Afisa habari huyo pia aLItumia fursa hiyo
kuwatahadharisha wanafunzi wa kike kuepuka ngono kwani kwa mujibu wa
utafiti wao takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike wenye umri wa miaka
15-19 wana uhusiano wa kingono na wanaume wanaowazidi miaka juu zaidi ya
umri wao hivyo kuwepo kwa hatari ya kuambukizwa VVU na Mimba za
utotoni.Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania
(UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga.(Picha zote na Malunde1 blog ya
Shinyanga)
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Busurwa,
Uhuru, Mazinge, Buluba, Chamaguha, Kizumbi, wakimsikiliza Afisa habari
kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi Usia Nkhoma
Ledama (hayupo pichani) ambaye alisema kwa mujibu wa sensa yao mwaka 2012
asilimia 65 ya Watanzania wote vijana wenye umri wa miaka chini ya
24,lakini pia asilimia 40 ya vijana wa kike wenye miaka chini ya 18
wanapata mimba za utotoni na wengine kuolewa katika umri huo.Aliongeza kuwa
asilimia 23 ya vijana umri wa miaka 15-19 wameanza kuzaa na katika umri huo
kati ya vijana wanne basi mmoja anaolewa ama kupata
mimba.
Wanafunzi wa vyuo vya VETA, MUCCOBS, Shycom ,
waliohudhuria katika warsha hiyo ya Umoja wa Mataifa wakimskiliza Afisa
habari kutoka UN, (hayupopichani) ambaye aliwataka kutumia fursa
mbalimbali zinazotolewa na Umoja wa mataifa hapa nchini,lakini pia kuwaomba
wazazi na walezi wa wanafunzi kujenga tabia ya kufuatilia mienendo ya
watoto wao na kuwasaidia ili kuwafanya wapende elimu ili kufikia malengo ya
Millenia.
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa
nchini Tanzania Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) alisema takwimu
zinaonesha kuwa asilimia 52 ya vijana wa kike umri wa miaka 18-14 wameanza
kufanya ngono na na asilimia 7 kwa wenye miaka 15-19 wanafanya ngono na
wanaume wanaowazidi umri miaka 10 zaidi ,huku vijana wa kiume wakidaiwa
kuanza kufanya ngono wakiwa na umri wa miaka 20, akatumia fursa hiyo
kuwataka vijana kuepuka ngono kwani wakindekeza ngono UKIMWI upo na
hawataweza kutimiza ndoto zao hivyo. Alisema Umoja wa Mataifa haupo tayari
kuendelea kuona vijana hawatimizi malengo yao.
Mjumbe wa asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa
Tanzania, Bw. Innocent akizungumzia kuhusu klabu za Umoja wa Mataifa katika
shule za sekondari na vyuoni ambapo alisema miongoni mwa faida ukiwa
mwanachama wa klabu hizo ni kupata taarifa nyingi tena kwa wakati kutoka UN
kuwa karibu na umoja wa mataifa, kuhudhuria mikutano ya UN, kupata nafasi
ya kusaidia jamii lakini pia kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali kama vile
kuongea mbele za watu,kuandaa ripoti,kupata vyeti
n.k
Walimu na wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo
wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika eneo la viwanja vya Mazingira
Senta mjini Shinyanga ambapo maafisa kutoka Umoja wa Mataifa walieleza kazi
za Umoja wa Mataifa na wakatumia muda fursa hiyo kuitaka jamii kubadilika
na kuhamasisha jamii kufuata uzazi wa mpango ikiwa ni pamoja na kuwa tayari
kupiga vita suala la vifo vya akina mama wajawazito na watoto,mimba za
utotoni ambapo watoto wa kike milioni 7.5 miaka chini ya 18 wanazaa kila
mwaka.
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda
ya ziwa (UNA), Bw.Moses Mongo akizungumza katika warsha eneo la Mazingira
Senta mjini Shinyanga ambapo alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1964
kote duniani na ndiyo taasisi pekee hapa nchini yenye klabu nyingi yenye
lengo la kuwaunganisha watu wa chini na Umoja wa Mataifa. Alisema hivi
karibuni wamefungua tawi la taasisi hiyo mkoani Shinyanga na mwenyeki wake
ni Bwana Ezra Manjerenga. Mosea Mongo alitumia fursa hiyo pia kuwataka
wanafunzi na wanajamii kwa ujumla kubadilika na kwamba mabadiliko yanaanza
kwa kutenda na wafanye kazi kwa malengo ili kuleta mabadiliko katika
jamii.
Bi
Usia Nkhoma Ledama akieleza kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa
Mataifa hususani malengo ya millenia kama vile kuhamasisha Afya ya Uzazi,
Haki za Binadamu, kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi, umaskini,
kuhamasisha Amani na Chakula kwa wenye njaa. Kulia ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga ndugu Anna rose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni
rasmi.
Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania
(UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga akimkaribisha mkuu wa wilaya
ya Shinyanga ndugu Annarose Nyamubi katika warsha hiyo iliyokutanisha shule
10 za sekondari na vyuo vitatu vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga.
Katikati ni Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania(UNIC) Bi. Harriet Macha na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi.
Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi, ambaye ni mdau wa maendeleo na
mwanafamilia wa Umoja wa Mataifa (siku za nyuma aliwahi kufanya kazi na
Umoja wa Mataifa katika shirika la UNICEF), alisema nchi ya Tanzania
inatekeleza malengo ya millenia kupitia ilani ya CCM katika kuwaletea
maendeleo wananchi wake hususani katika kupunguza
umaskini.
Katika hatua nyingine Bi. Nyamubi aliwataka vijana
kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa mataifa. Mkuu huyo wa wilaya
aliongeza kuwa serikali inawajali vijana hivyo kuwataka kusoma kwa malengo
kwani bila elimu dunia itawaacha na kuwataka kuacha kutegemea wazazi wao
kwamba watarithi mali.
Aidha Nyamubi alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi
ambao hawajapeleka watoto wao kidato cha kwanza wawapeke haraka kabla ya
kuwachukulia hatua.
Mapema kabla ya warsha Afisa habari kitengo cha
habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha ambapo alisema
lengo la ziara yao ni kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za Umoja wa Mataifa
na kutoa elimu kuhusu shughuli za Umoja wa Mataifa ambapo huwa wanatembelea
shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kuwaelimisha kuhusu ajenda za
Umoja wa Mataifa.
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA), Bw.
Moses Mongo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha
iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema shule hiyo ni miongoni
mwa shule chache zilizopata bahati kutembelea na Umoja wa mataifa na
kuwataja miongoni mwa watu ambao ni mazao ya klabu za Umoja wa Mataifa kuwa
ni Zitto Kabwe na John Mnyika.Alisema klabu za Umoja wa Mataifa
zinawajengea wanachama wake ujasiri pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali
kama vile elimu ya ujasiriamali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Chamaguha wakinyoosha
mikono kwamba wako tayari kuwa na klabu ya Umoja wa mataifa katika shule
yao baada ya kuridhishwa na maelezo kutoka Umoja wa Mataifa hapa nchini
wakiongozwa na Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa Tanzania
(UNIC)Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Awali katika shule ya sekondari Chamaguha katika
manispaa ya Shinyanga ,ambako maafisa wa Umoja wa Mataifa walifanya ziara
yao, Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania
(UNIC) Bi. Harriet Macha akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambao
wamedhamiria kuanzisha klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule hiyo ambayo
itaundwa na wanafunzi kuanzia 10 na kuendelea .Hapo anaonesha vitabu na
vipeperushi mbalimbali vinavyohusu Umoja wa Mataifa ambao ulianzishwa mwaka
1945 baada ya vita ya pili ya dunia.Hivi sasa Umoja wa Mataifa una nchi
wanachama 193 duniani kote na nchi 3 pekee siyo nchi wanachama wa Umoja
huo, nchi hizo ni Taiwan,Cossovo na Vatican.
Ni
katika ofisi ya walimu katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa
ya Shinyanga,muda mchache tu baada ya maafisa kutoka Umoja wa mataifa
kuwasili katika shule hiyo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Aliyesimama ni kaimu mkuu wa shule hiyo bwana Malongo Maganga
akiwakaribisha wageni hao ambapo aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuwafikia
na kufurahishwa na mpango wake kuhusu elimu ya uzazi wa mpango kwa
wanafunzi kwani itawasaidia kuongeza uelewa na kujilinda zaidi ili kutimiza
malengo yao.Alisema jamii inaamini kuwa elimu hiyo ni kwa ajili ya akina
mama pekee.
Aidha mwalimu Maganga alisema tayari shule yake
imefungua faili kwa ajili ya klabu ya Umoja wa Mataifa kwa wanafunzi wa
shule hiyo.(Picha zote na Malunde1 blog ya
Shinyanga)


















0 comments