Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank
Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es
Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili. Kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe.(Picha na Zainul
Mzige).
Na
Damas Makangale, MOblog
HUKU
Tembo wakiendelea kuuawa katika mbuga kadhaa nchini, Serikali ya Ujerumani
imeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kupambana tatizo la ujangili
Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard
Membe amesema serikali ya ujerumani imeahidi kutoa msaada wa vifaa na ujuzi
wa kupambana na ujangili katik mbuga za Tanzania.
"tupo
katika hatua za mwisho za ushirikiano wa kupambana ujangili na majangili
ili kunusuru Tembo wetu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo," amesema
Membe.
Waziri
Membe amesema kwamba serikali ya Ujerumani imetoa magari ya kupambana
ujangili, camera, vifaa vya kisasa na mafunzo kwa askari wa wanyamapori ili
kuwajengea uwezo wa kupambana na majangili nchini.
Picha juu na chini ni Baadhi ya wageni waalikwa na
maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani
nchini.
Amesema tatizo la ujangili si la Tanzania peke yake
linahitaji ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika na ulaya kwa sababu
pembe za ndovu kuuzwa kwenye nchi hizo au kuwa kama njia ya
kupitishia.
"wanatoa mafunzo ya kutosha kwa askari wetu wa
wanyamapori ili waweze kukabiliana kikamilifu na majangili,"
aliongeza
Waziri
Membe alizungumza kwenye mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya nchi za
Nje wa Ujerumani Dkt Frank-Walter Steinmeier ambaye alitembelea nchini kwa
mara ya kwanza tangu kushika nyadhifa hiyo
Kwa
taarifa ambazo zipo ni kwamba Tembo 25,000 waliuawa mwaka 2011 na 22,000
waliuawa mwaka 2012, ni ishara inayoonyesha kuwa biashara haramu ya wanyama
pori sasa imekuwa ni uhalifu wa kidunia wenye nguvu ya kuathiri maendeleo
ya kiuchumi, kusababisha migogoro, kuimarisha vikundi vya kigaidi na
kuathiri watu wenye hali duni ya watu waishio katika
umaskini.
Faru
wanauawa na maharamia kila baada ya dakika 10 na ni wachache kuliko chui
3,500 ambao wamebaki porini.
Ujangili unaathiri jamii barani Afrika, hususan yale
maeneo katika bara ambapo wanakabiliwa na hali mbaya ya janga la ujangili.
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na
waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo jijini
Dar.







0 comments