Friday, 28 March 2014

NIGERIA YAOMBA UMOJA WA MATAIFA USAIDIE MAPAMBANO DHIDI YA BOKO HARAMJ

By    
Jan Eliasson
Spika wa baraza la juu la bunge la Nigeria David Mark ameomba uingiliaji wa Umoja wa Mataifa katika kupambana na kundi la waasi la Boko Haram.
Mark alisema hayo huko Abuja baada ya kukutana na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson, ambaye yuko ziarani nchini Nigeria. 
Mark amesema, Nigeria inahitaji uungaji mkono na msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto ya usalama. 
Aidha, Mark aliongeza kusema Nigeria itaendelea kufanya kazi muhimu katika mambo ya kimataifa na ya kikanda, kwani nchi hiyo ina rekodi nzuri katika operesheni ya kulinda amani.


CHANZO: AHBAAUR RASUUL

0 comments