Tuesday, 25 March 2014

VIONGOZI WA KIISLAMU KENYA WATAKA WANAWAKE WAUNGE MKONO MSWADA WA NDOA ZA WAKE WENGI

By    
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfpWT7nYZV6x963hB3j1MLeu0zw5coBGCYi4gnAuyWGDIfv5x2zYaHSyVzNYWbmuoke2pIEQ_cuaLefdU3WQCDIm4buzOHgNP9roeIhJi_aoMAKsQAwu9ch_GKyO5UcOEytlTzK6V3NlSa/s1600/sheikh%20m%20khalifa.jpg
VIONGOZI wa Kiislamu Jumapili wamewasisitiza wanawake kukubali mswada wa ndoa uliopitishwa na wabunge mnamo Alhamisi wakisisitiza utawapa fursa bora na kuwabana wanaume wanaopenda kuchezea wanawake.
Wakiongea na vyombo vya habari katika ofisi zao eneo la Mwembe Tayari, viongozi wa Baraza la maimamu na wahubiri (CIPK), waliwataka wanawake kutokuwa na wasiwasi kwani mswada huo unawalinda.
Katibu wa CIPK Sheikh Mohammed Khalifa alisema, waislamu wana sheria zao kuhusiana na talaka, urathi na ndoa. Alisema Kislamu mwanaume anaruhusiwa kuoa bila ya idhini ama ruhusa ya mke wa kwanza kwa mujibu wa Quran.
Sheikh Khalifa aliwataka wanawake kuunga mkono mswada huo kwa kusema  kuwa, ”Kwa Quran mwanaume anaruhusa na idhini ya kuoa bila ya ruhusa ya mke wake wa kwanza na wanawake wa kikistro mjue kwamba, wanaume hawatowachezea tena. Tunampongeza Bw Duale kwa kupigania mswada huu”.

0 comments