Friday 17 October 2014

REDIO JAMII ZISIKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA KWA MANUFAA BINAFSI

By    
DSC_0043
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi kuzungumza na washiriki 31 wa mtandao wa redio jamii Tanzania (COMNETA) unaotekeleza mradi wa demokrasia na amani (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu 2015 wanaohudhuria warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amezitaka Redio za Jamii kutokubali kutumiwa na vyama vya siasa vinavyotumia unyonge wa watanzania kiuchumi kujinufaisha kisiasa.
Alisema kwa kufanya maamuzi ya kutotumiwa na vyama vya siasa kutasaidia kuepusha migogoro inayochochewa na taarifa za kishabiki za vyamja vya siasa.
Jaji Mutungi alisema hayo wakati akichangia mada tatu zinazohusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi 2010, Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya vyama vya Siasa zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii nchini katika warsha inayoendelea mjini hapa.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo ya siku nne inayohusu utekelezaji wa mradi wa kuendeleza majadiliano kwa njia ya amani kwa lengo la kukuza demokrasia nchini,kutambua kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia unyonge wa kielimu na uchumi wa watanzania kuwaahidi mambo yasiyotekelezeka jambo ambalo amesema ni matumizi mabaya ya uhuru wa taasisi.
DSC_0073
Msaajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi akizungumza na wadau wanaohudhuria warsha ya siku nne ya kutekeleza mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) inayoendelea mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) Bwana Al Amin Yusuph na Katikati ni Msajili msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa.
Alisema vyombo vya habari vya jamii bado visafi na vina nafasi kubwa kubadilisha mitazamo ya utamaduni wa siasa chafu iliyojengeka kuwa maendeleo ni kupata uongozi wa siasa, tena kwa kauli za uwongo na kujenga chuki.
“Maendeleo ni kuchagua kiongozi ambaye ni mwadilifu, mwenye uchungu na taifa na yuko tayari kuitunza amani tuliyoirithi baada ya kupata uhuru wa nchi.” alisema Jaji Mutungi.
Mada hizo ziliwasilishwa na Wasaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa Ibrahim Sapi Mkwawa, Sisty Leonard Nyahoza na Ofisa Sheria Mwandamizi Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi vya Siasa.
Msajili wa Vyama Vingi amesema, kwa kuwa Redio Jamii ndiyo zinazowafikia watanzania wenye maisha ya kawaida walio wengi vijijini na ndio wanaofuatwa na wanasiasa wa namna hiyo ili wawaunge mkono nia zao bila kujali maslahi ya wananchi.
DSC_0246
Wadau wa mradi wa uchaguzi wakifurahi jambo wakati Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Amezitaka redio jamii kuunganisha nguvu ya pamoja na wadau wakuu wa mradi wa uchaguzi kwa kuwaelimisha wananchi, kusema ukweli bila woga kitu chenye manufaa kwa umma hasa kuhusu wanasiasa matajiri kutumia raslimali zao katika kutafuta kura hali ambayo imeliingiza taifa katika wimbi la rushwa na umaskini wa kupindukia.
Alisisitiza kuwa siasa ni ushindani na kushinda hivyo zisirubuniwe kirahisi kwa pesa ambazo sio msingi wa maendeleo.
“Pesa sio msingi wa maendeleo, msikubali kurubuniwa wala kununuliwa na wachache wanaotumia nguvu ya pesa. Silaha kubwa ni kuunganisha nguvu na vyombo vya habari jamii tutafanikiwa kulijenga taifa.”
Wakati huo huo ofisi ya Msajili wa Vyama Vingi imekuwa ikikabiliwa na matatizo kutokana na udhaifu wa sheria ambao wanasiasa wamekuwa wakiutumia kwa kutoa lugha chafu na za uchochezi ili waweze kuungwa mkono bila kujali maslahi ya taifa.
DSC_0094
Msajili msaidizi kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa, akiwasilisha mada ya Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 kwa wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) kwenye warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma. Kutoka kulia meza kuu ni ........Sisty Leonard Nyahoza, Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji John Mkwawa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo.
Mada nyingine iliyotolewa katika mkutano huo wa siku nne uliofadhiliwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP na UNESCO iliyofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu mjini Dodoma ni Jinsia na Kuhusisha Makundi Maalum Katika Uchaguzi 2015 na Margareth Rugambwa kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Kuwapatia Uwezo Wanawake (UN Women).
Katika semina hiyo washiriki wameazimia kutumia redio jamii katika kufanikisha mawasiliano baina ya wananchi na vyombo vinavyosimamia masuala ya uchaguzi na siasa.
DSC_0133
Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza, akiwasilisha mada ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa wadau wa warsha ya mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu mwakani inayoendelea mjini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
DSC_0124
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku nne kwa wadau wa mradi wa uchaguzi 2015 unaolenga kuboresha demokrasia amani nchini (DEP)katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) iliyoenda sambamba na mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA).
DSC_0139
Afisa Sheria Mwandamizi Piencia Etanga kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akiwasilisha mada ya Kanuni za Maadili ya vyama vya Siasa zilizotolewa kwa viongozi na wamiliki wa redio jamii nchini katika warsha inayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0002
Msajili msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wasaidizi wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa (kushoto) kwenye washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
DSC_0028
Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, akielezea utekelezaji wa mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini chini ya ufadhili wa UNDP kwa wadau wa redio za jamii nchini.
DSC_0015
Katibu wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA), Bw. Abbas Mwakalinga (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Bw.Joseph Sekiku wakati wa warsha hiyo.
DSC_0225
Meneja wa Pambazuko FM Radio ya Ifakara, Bw. Joseph Kamata akihoji swala kwa wa wasilishaji mada kwenye warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma.
DSC_0127
Kutoka kushoto ni Mshauri wa UNESCO na Mlezi wa mtandao wa redio jamii (COMNETA), Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu pamoja na Afisa Habari na Mahusiano Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
DSC_0199
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini (RPP), Jaji Francis Mtungi akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha ya siku nne inayoendelea mjini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu.
DSC_0186
Mshauri wa UNESCO na Mlezi wa COMNETA, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph wakati wakielekea kupiga picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
DSC_0168
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi akifurahi jambo na rafiki yake wa siku nyingi Reportuer wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi inayoendelea mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo.
DSC_0172
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mtungi, wakufunzi, wafanyakazi wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki.
DSC_0176

0 comments