Wednesday 15 October 2014

SHULE 30 ZAUNGANISHWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LISILO LA KISERIKALI LA ACTIVISTA TANZANIA PAMOJA NA ACTION AID KUWEZA KUWAFAHAMISHA KUHUSU NGUVU YA KODI KWA VIJANA

By    
Mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo  akifungua bonanza la NGUVU YA KODI lililofanyika katika Viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii katika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipofariki  Dunia  Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limemkumbuka Baba wa Taifa kwa kutoa Elimu na maelezo ya kutosha juu ya Kodi na Nguvu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu na Kukuza uchumi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo (kushoto) akiwa na Mratibu wa Shirika La Activista Ein Ahimidiwe wakati akimkaribisha kusaini katika ubao wa saini
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akisai ubao kuungana na Activista pamoja na Action Aid Tanzania katika upingaji wa watu kuto kulipa kodi
Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bw.Salehe B Msholo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika bonanza akitia Saini yake katika ubao wa saini katika uwanja wa ustawi wa jamii siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia  Jijini Dar es Salaam 
 LRP Coordnator&Partnership Develop[ment manager Jovina Nawenzala Akitia saini katika ubao wa saini ili kuunga mkono wanafunzi wanaopinga  kutokulipa  kodi kwa baadhi ya wawekezaji na wengine kuwekewa punguzo la kodi
Bi. Jovina Nawenzala akitoa ufafanuzi wa kina kuhusu shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la Action Aid na kazi zake katika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia 
Mabango mbalimbali yakiwa na  na ujumbe tofauti katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipofariki Dunia 
 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la maendeleo la kabenzo Tanzania john A Sekamba Kulia akiwa na Jerry Kerenge katika bonanza hilo
 
Watumbalimbali walio ungana na kuweza kuweka saini katika ubao ilikuweza kukumbusha  watu kulipa kodi ndio maendeleo ya nchi yetu
Vikombe vikiwa mezani vikisubiri mshindi katika mpira wa miguu pamoja na mpira wa pete kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa vyuo na shule za sekondari
Mechi kati ya chuo cha ustawi wa jamii wakiwa wanapambana vikali na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere
 Wanatimu kwa upande wa vyuo walioshinda  na kuondoka na kikombe kwa mshindi wa kwanza ni chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 
Mlinda mlango wa timu ya shule ya sekondari oysterbay  akiupangua Mkwaju wa penati na kuipelekea timu yake kuwa mshindi na kutinga nusu fainali
 Baadhi ya Timu shiriki katika mashindano yaliyo andaliwa na Action Aid na Activista Tanzania 
Mchezo wa kuvuta kamba nao haukuwa mbali hizi ni baadhi ya timu chache shiriki
wanafunzi mbalimbali wakijiandaa kukimbia mbio za urefu wa mita miamoja
 Mshindi wa mbio za mita Miamoja (100)kwa wanafunzi wa kiume Japhet Mwandimo kutoka shule ya sekondari Kibasila
  Mshindi wa mbio za mita Miamoja (100) mwanafunzi kwa wasichana Salome Saimon akisai jina lake baada ya kuibuka mshindi
Timu ya washindi wa mchezo wa mpira wa pete katika bonanza hilo katika shule ya sekondari wakiwa katika picha ya pamoja
Mgeni Rasmi Akimkabidhi Mwakilishi wa mshindi wa pili katika mchezo wa mpira wa pete kutoka chuo cha ufundi Veta akipokea medani kwa niaba ya Timu
 Mshindi wa mbio za Ndimu Akipokea Medali Ya ushindi wa Mbio hizo katika Bonanza kutoka kwa mgeni rasmi
 Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bw.Salehe B Msholo ambaye ndiye Mgeni Rasmi akifunga Bonanza lililofanyika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia  Jijini Dar es Salaam 
 Picha za pamoja waalimu wafanyakazi wa mashirika wanafunzi pamoja na Mgeni Rasmi
Baadhi ya wanafunzi walio weza kuhudhuria bonanza hilo 
  kikundi cha burudani kikiwa kipo jukwaani kwaajiri ya kusherehesha katika bonanza lililo andaliwa na Action Aid Tanzania 


0 comments