Friday, 24 October 2014

YOA KUWATUZA WASANII

SHIRIKA la kitaifa linaloongoza vijana (Yoa) wanatarajia kutoa tuzo kwa vijana chini ya miaka 30 waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali za sanaa nchini.

Tuzo hizo zitatolewa kupitia vipengele 15 vilivyoandaliwa ikiwemo vya kilimo, uvumbuzi, mchango jamii, uanamitindo, uchapishaji, ujasiriamali, muziki, uigizaji.

Pia katika kipengele cha utangazaji, wazo la biashara, mchango wa jamii, ubunifu mitindo, tovuti bora na taaluma.

Mkurugenzi wa Yoa, Harrison Mbugi aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa tuzo hizo zinalenga kutambua vijana wa kitanzania walio chini ya miaka 30 na kuwatia hamasa ili wazidi kuwa na ndoto endelevu na kuondokana na tatizo la ajira nchini.

Alisema ni mara ya kwanza kwa Yoa kutoa tuzo hizo na kwamba zinawalenga vijana moja kwa moja.

“Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Uongozi Institute, Africa Media Group (Channel Ten na Magic FM), Fastjet na nyingine ambazo zimetupa nafasi ya kuandaa tuzo hizo ili kutimiza malengo ya vijana nchini,” alisema Mbugi.

Aliongeza kuwa muda wa kutoa tuzo hizo haujafahamika kwa kuwa upendekezaji wa majina hayo bado unaendelea hadi Novemba 10, mwaka huu.

Akizungumzia vigezo kuhusu tuzo hizo, Mbugi alisema washiriki wanatakiwa kuwa na umri chini ya miaka 10 na walio na mafanikio kupitia vipengele vilivyoainishwa.CHANZO: HABARU LEO

0 comments