
Tofauti na wengi wanavyodhani, mzee wangu Pinda ulishaonyesha dalili za wazi ikiwa kweli unamudu vyema nafasi ya uwaziri mkuu. Kuna mengi tu yaliyofanya baadhi yetu tutilie shaka umahiri wako lakini hii skandali ya Tegeta/Escrow imefunga mjadala!
Unakumbuka uliposema na wapigwe tu? Liwalo na liwe! Wakumbuka ile kauli ya tumechoka? Wakumbuka mgomo wa madaktari? Je wakumbuka kauli yenye utata “anayeua albino na yeye auwawe”? Lakini wajua namna “mchwa” katika baadhi ya halmashauri wanavyotafuna fedha za wananchi?
Tegeta/Escrowni hitimisho la yote haya, mzee wangu Pinda mtoto wa kulima, let it go! Jiuzulu, mpe fursa rais Kikwete aunde baraza jipya la mawaziri, urais unaweza kutafutwa hata nje ya uwaziri mkuu!
Ukiwa mwanasheria utanielewa vizuri naposema hoja si ikiwa unahusika au la! Hili si muhimu sana, hoja hapa ni dhamana ya uongozi kusimamia shughuli za serikali ilishindwa kutumika kunusuru “skandali”hii. Kiongozi waumma “kutuhumiwa” si jambo jema, tuhuma pekee zinatosha kukufanya ubwage manyanga “resigning does not mean you are weak, but sometimes it means you are strong enough to let it go”
Achia ofisi ya umma kwa manufaa ya walala hoi wa Tanzania, kiongozi wa umma umetuhumiwa kutosimama kidete kuzuia uozo huu kabla, kauli za “kila mtu atabeba msalaba wake” si za kulisaidia taifa, ni kauli inayoashiria hamu ya mtawala asiyependa kuwajibika, anayetaka kung’ang’ania madaraka! Haifai kabisa, busara inakutaka kuwajibika kama mtangulizi wako Edward Ngoyai Lowassa, kumbuka “Caesar’s wife must be above suspicion’’
novakambota@gmail.com , http://novakambota.wordpress.com



0 comments