Saturday 22 November 2014

KAWAMBWA: MAFANIKO YA MUHITIMU HAYAPIMWI KWA MITIHANI

By    
Waziri wa elimu Dr. Shukuru Kawambwa amesema kuwa mafanikio ya muhitimu hayapimwi kwa mitihani badala yake yanapimwa kwa juhudi, maadili na utumiaji wa elimu yake aliyoipata katika maeneo ya kazi.

Kawambwa ameyasema hayo hii leo katika mahafali ya kwanza ya chuo cha uhandisi na teknologia cha Al-maktoum kilichopo Mbezi beach jijini Dar es salaam, alipokuwa anawatunuku veti wahitimu 87 katika ngazi ya stashahada na cheti katika fani za electical, electronic na Information technology.

Katika mahafali hayo yaliyofunguliwa na mwenyekiti wa bodi ya Al-maktoum Profesa Hamisi Ndihenga, ambapo alitoa maelezo mafupi kuhusu Al-maktoum ambapo Mkuu wa chuo hicho Dr. Hamdun Ibrahim Sulayman alieleza kwa ufupi historia ya chuo hicho na kuzungumzia matarajio yao ya muda mfupi na mrefu wa chuo hicho.

Mheshimiwa Kawamaba katika kuwataka viongozi wa Al-maktoum kuzidisha ubora wao alisema kuwa hakuna mwisho wa maboresho ya mambo na kuwataka viongozi kuongeza wigo na ikiwezekana kuwepo pia na madarasa ya jioni 

Kawambwa amesema kuwa nchini inahitaji zaidi mafundi kuliko maengineer na kuwataka viongozi wa Al-maktoum kujikita zaidi katika utoaji wa stashahada kuliko kukimbilia kuto shahahada katika fani wanazo zitoa.
Wahitimu waliopewa vyeti vyao hii leo
Kawambwa alisema kuwa Engineer mmoja anahitaji matechnician 25, ambapo kwa sasa nchini hakuna uhiano huo unaotakiwa, na kilicha sababisha hicho ni kitendo cha vyuo vingi kujikita katika utoaji wa shahada katika fani hizo.

Muheshimwa Kawamba alisema kuwa matechnician ndio watendaji wa kuu katika taasi mbalimbali na hupelekea mahala pemgime kuitwa maengineer, hivyo technician ni mtu muhimu katika ukuwaji wa taasisi pamoja na nchii kwa ujumla.

Katika ushahuli wake kwa wanafunzi waliobaki Muheshimu Kawambwa aliwataka Wanafnuzi hao kujikita katika kusoma na kuwataka wahadhiri wajikiti katika kuelekeza na si kujipamba kwa kuwapigisha wanafunzi supplimentary na disco.
'Umahili wa muhadhiri sio katika kuwakamata mwanafunzi katika supp na disco', alisema Kawambwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa chuo Dr Hamduni alielezea fursa iliyoitoa Al-maktoum kwa wanafunzi waliofanya vibaya katika mitihani yao ya kidato cha nne kwa kuwapa kozi ya veta kabla ya kuingia katika upande wa cheti na kujiendeleza mbele kadri awezavyo.

Dr. Hamduni alisema kuwa wamefikia uwamuzi wa kuanzisha veta chuoni hapo baada ya kubaini kuna vijana wengi wanashindwa kujiendeleza kwa matokeo mabaya waliyo yapata katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Al-maktoum kina miaka minne toka kuanza kwake wakiwa wametoa toleo nne katika ngazi ya cheti na toleo la kwanza katika upande wa stashahahda.bora ni 






0 comments