Sunday 23 November 2014

MSUNI: KUFELI SI MWISHO WA KUJIENDELEZA KIELIMU

Msuni akingoja kukabithiwa cheti
Mmiliki wa blog za Tembezi za Msuni, Sport In Bongo na Chama langu ni Azam, Abdallah H.I Sulayman "Msuni" amewataka wanaofeli mitihani yao wasiwakate tamaa.

Msuni aliyasema hayo jana katika mahafali ya kwanza ya chuo cha uhandisi na teknologia cha Al-Maktoum pale alipohojiwa na kituo cha utangaza cha Taifa TBC1, mara baada ya kumalizika kwa mahafali hayo.

Msuni alisema kuwa kufeli katika mtihani wa kidato cha nne si mwisho wa kujiendeleza kielimu kwani unaweza kufikia malengo yao ya kupata shahahda yako kwa kuanza na kozi ya veta kisha cheti, stashahada na kufikia pale ulipo palenga.

Kauli ya Msuni ilikuwa inajazia maneno yaliyo semwa na mkuu wa chuo hicho Dr. Hamdun Ibrahim Sulayman alipozungumzia kwanini walifikia uwamuzi wa kuanzisha kozi za veta chuoni hapo.

Dr. Hamduni katika risala yake alisema kuwa uwepo wa kozi yav veta chuoni hapo ni nafasi nyingine kwa mwanafunzi waliofeli kidato cha nne katika kujiendeleza kielimu.

Dr. Hamdun aliwataka wazazi kuwapa nafasi nyingine wanafunzi wanaofanya vibaya katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Msuni akiwa na mwalimu wake Ramadhan
Msuni ni miongoni mwa wahitimu 87 waliopewa vyeti vyao hiyo jana huku Msuni akiwa ni kati ya wanafunzi 13 walihitimu ngazi ya stashahada katika fani ya Information Technology, huku walihitimu katika fani ya Umeme katika ngazi ya stashahada wakiwa 10, na waliosalia ni wahitimu wa ngazi ya cheti katika fani za Information Technology, Elctical na Electronic.
Msuni sambamba na Mke wake mara baada ya mahafali kumalizika

Msuni akilishwa keki na muhitimu mwenzake katika fani ya Information Technology, Halima
Msuni akiwa sambamba na Habib Khamis (Alipta kuwa mshirika wa Msuni katika kitengo cha Msuni Computer solution)pamoja na mke wa Msuni

Picha ya pamoja, Msuni akiwa kachuchuma mbele ya mgni rasmi, Mheshimiwa Shukuru Kawambwa

0 comments