Sunday, 16 November 2014

SIMULIZI: MSOMI NA ASIYEMSOMI

By    
Ona hii Msomi mmoja mwenye PhD pamoja na kijana mmoja ambaye hakubahatika kusoma walisafiri pamoja kwenda kutembelea mbuga moja maarufu yenye maua na ndege wa kuvutia.

Usiku ulipofika wakaweka hema lao zuri na la kisasa na wakalala usingizi mzito kabisa.

Masaa machache baadae, Yule kijana asiye msomi akamuamsha yule msomi na kumwambia 'hebu angalia angani kisha niambie umegundua nini?'

Jamaa mwenye PhD aka jibu: "Naona mamilioni ya nyota na mbalamwezi.'

Yule kijana asiye msomi akauliza tena "Unajifunza nini ukiona hivyo?"

Msomi akatafakari kwa dakika kadhaa kisha akajibu: "Upande wa kiunajimu inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi sana katika hii dunia kwetu wanadamu..... Upande wa muda inaonyesha ni usiku wa manane....Upande wa imani inadhihirisha kuwa Mungu ni muweza wa vyote na sisi kwake ni viumbe wadogo sana na tusio na mamlaka... Upande wa hali ya hewa.... kesho itakuwa siku nzuri sana".

PhD kisha naye akauliza.... kwa upande wako wewe umegundua nini?"

Yule jamaa asiye msomi akakaa kimya kwa muda na kisha akajibu: "Kiuhalisia....mimi nimegundua kuwa ...Hema letu limeibiwa!!

0 comments