Tuesday, 30 December 2014

BEKI TATU YAJA

By    
KIKUNDI cha Sun Shine Artists Theatre chenye makao yake makuu Ilala, jijini Dar es Salaam kimetayarisha sinema inayoitwa Bekitatu inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni.

Kwa mujibu wa maelezo ya mtayarishaji wa sinema hiyo, Haji Dilunga, Beki tatu inaelezea na kutoa taswira ya jamii ya kitanzania inavyoishi na wafanyakazi wa ndani.
“Ni sinema inayofichua siri nzito ya maisha ya wafanyakazi wa ndani na mabosi zao,” alisema.

Katika sinema hiyo, Mwanadada Nurati Ngeleshi amecheza kwa jina la Rukia, akiwa na watoto wake ambao ni Nurdin Salum aliyecheza kama Jaffary.

Clemensia Salum aliyecheza kama Leila, Hassan Lukuu aliyecheza kwa jina la Bakari akiwa kama mdogo wake Rukia. Mwingine ni Hawa Hassan aliyecheza kwa jina Sikitu au Bekitatu, katika sinema hiyo amecheza kama mfanyakazi wa ndani wa familia ya Rukia.

“Sinema inafumbua fumbo la kwanini wafanyakazi wa ndani wanatokea kutenda vitendo vya kikatili kwa mabosi wao... “Sidhani kama wewe mpenzi wetu utakuwa unafahamu, jibu lake ni kutafuta sinema hiyo utafahamu kwanini wafanyakazi wa ndani wanatenda vitendo vya kikatili kwa mabosi zao. Ni sinema inayosikitisha na kuhuzunisha, wakati huo huo kufurahisha na kutoa elimu kwa jamii,” alisema Dilunga.

Sinema hiyo imetungwa na kuandikwa mwongozo na Dilunga, inasambazwa na kampuni ya BMO ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya sinema zilizoandikwa na Dilunga na Kwanini Mama? Jamila, Pete ya Ajabu, Mwandishi, Sound of Death na sasa anakuja na Beki tatu.

“Usiogope kununua kwa vile imechezwa na waigizaji wachanga, nunua ili upate uhondo na kutambua uwezo wa waigizaji wanaochipukia katika ulimwengu wa sinema,” alisema.

0 comments