MW A N A D A D A anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kamwe hatarajii kujiingiza katika masuala ya siasa kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kuwa kwake siasa ni kitu aambacho hajawahi kukifikiria.
“Binafsi sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao,” alisema Lady Jaydee.
Alisema anafurahi kufanya mziki na wala hajutii kwa kuwa unamuongezea kipato kikubwa na ataendelea kutunga nyimbo zenye maudhui na mvuto na kwa wakati husika.
Baadhi ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Haule ‘Profesa J, Khadija Shabani ‘Keisha’ na Ummy Wenslaus ‘Dokii.



0 comments