Mkuu wa wilaya ya Masasi Farida Mgomi amesema hayo mjini Masasi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ukaushaji wa samaki kwa kutumia nishati ya jua yaliyoshirikisha washiriki 20 kutoka Somanga wilaya ya Kilwa mkoani Lindi ambapo ametaka mafunzo hayo kuchangia kuboresha shughuli za uvuvi kwenye maeneo ya bahari ya Hindi na hivyo hivyo kukuza soko la samaki na kuchangia katika maendeleo ya jamii na kupunguza umaskini wa kipato.
Mratibu wa mafunzo hayo FRED MWAKAGENDA amesema mafunzo hayo yana lengo la kusaidia uboreshaji wa kukausha samaki na kupunguza uharibifu wa mazingira pamoja na kuongeza ushindani wa soko kwa wajasiliamali.
0 comments