Monday 22 December 2014

JOHNSON LUKAZA WA KESI YA EPA ASHINDA KESI

By    

https://m.ak.fbcdn.net/photos-e.ak/hphotos-ak-xfa1/v/t1.0-0/p320x320/1606874_782111758527481_8821923949285361956_n.jpg?efg=eyJpIjoiYiJ9&oh=ea6494f41da148aacb6840164d4688af&oe=550A2B9B&__gda__=1426553077_c47ae4a35693f409fafa75038a118871

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachiria huru Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdomo wake Mwesigwa Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.

Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.

Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi

0 comments