Katika mchezo huo wa jana uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ulisihuhudia Taifa stars maboresho wakicheza bila maelewano yoyote na kama Burundi wangezitumie vyema nafasi walizo pata wangeweza kupata ushindi wa kuanzia goli 4.
Taifa stars ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Yusuph Rashid akiunga kwa kichwa krosi ya Kelvin Friday katika dakika ya 11 ya mchezo.
Kipindi cha pili kiliendelea kutawaliwa na Burundi na kufanikiwa kupata goli la ushindi na kupelekea mchezo kumalizika kwa Burundi kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Burundi wamecheza na Tanzania mara tatu katika mwaka huu na kufanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yote mitatu, ambapo Burundi walichapa Taifa stars maboresho goli 3-0 mchezo uliochezwa aprili 26 mwaka huu katika uwanja wa taifa, kabla ya kuwafunga Taifa stars goli 3-0, mchezo uliochezwa nchini Burundi na jana kuwafunga goli 2-1.



0 comments