Friday 16 January 2015

THT KUWASAIDIDIA VIJANA WABUNIFU

NYUMBA ya Vipaji Tanzania (THT) inaadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa kwake ambapo imetangaza rasmi mpango wake mpya wa kuwainua vijana wabunifu na washonaji wa nguo kwa kutumia vitenge.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Januari 31 mwaka huu katika ufukwe wa Escape One na kushirikisha wasanii mbalimbali wa muziki waliolelewa THT na wengine ambapo wataimba muziki wa bendi.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 walikuwa wana lengo la kuinua vipaji vya vijana wanaopenda muziki zaidi ya 3,000 ambao walikuwa hawana uwezo kifedha, lakini sasa mpango huo umesimamishwa rasmi na kusema kuwa watakuwa wakifanya kazi na wanamuziki wanaojua.

Akizungumza jana kuhusu maadhimisho hayo Meneja Mkuu wa THT Mwita Mwaikenda alisema vijana wa kike na kiume ambao wanapenda kujifunza mitindo watakuwa wakipewa mafunzo hayo bure yatakayokuwa yakisimamiwa na Mwanamitindo mashuhuri nchini Ally Remtullah.

"Ndani ya miaka ya 10 tumewasaidia vijana wengi tumewafundisha muziki baadhi yao ni Linah Sanga, Amini Mwinyimkuu, Elias Barnabas na wengine zaidi ya 3,000 leo wana maisha yao," alisema.

Mwaikenda alizungumzia mafanikio waliyopata tangu kuanzishwa kwa THT, ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kurekodi muziki, studio ya kutengeneza vipindi, wamekuwa wakitengeneza matangazo na kufanya kazi na kampuni mbalimbali za biashara.

Alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwaunga mkono wazo lao la kuwasaidia vijana wanamuziki ambapo wengi wamenufaika na wanategemea sanaa hiyo kuendesha maisha yao ya kila siku.

Naye, Mwanamitindo maarufu nchini Remtullah alisema ujio wa THT katika kuwainua vijana.

0 comments