Hoja kuwa tokea yawasili nchini mwezi Desemba , 2014 hayajaanza kutumika kwa vile ni mabovu ni upotoshaji wa ukweli. Ukweli ni kwamba kuanzia Novemba 24, 2014 TRL ilipeleka maombi katika Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini –SUMATRA ya kuruhusiwa kuanzisha huduma ya treni ya abiria ya “deluxe’ kwa kutumia mabehewa hayo na kutoza nauli maalum.
Februriari 25, 2015 Sumatra imetoa idhini ya kuanzisha huduma hiyo kwa kuyatumia mabehewa hayo 22 baada ya kutimiza masharti ya uendeshaji. Hivi sasa TRL inakamilisha masharti hayo na safari ya kwanza ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika Aprili 1, 2015 kwenda Kigoma kupitia katika stesheni zilizoainishwa katika jedwali la nauli ambalo limekuwa likitangazwa na baadhi ya magazeti tokea wiki iliyopita.
Kuhusu kadhia ya ubovu wa mabehewa aina mbalimbali yakiwemo yale 25 ya kubebea kokoto BHB, 50 ya kubebea Makasha CCB, 100 ya kubebea mizigo ya kichele CLB na 17 ya breki BVB haya yote yamenunuliwa kwa mikataba maalum ambayo imeweka masharti kwa gharama za mtengenezaji kuyafanyia marekebisho endapo hitilafu zitajitokeza wakati kipindi cha majaribio. Aidha mikataba yote imetoa dhamana ya kati ya mwaka mmoja na miwili kwa ajili kurekebisha hitalafu zozote zitakazojitokeza wakati wa matumizi ya vitendea kazi hivyo.
Kwa taarifa hii tunawaomba tunawahakikishia wananchi wote kuwa mabehewa ya abiria yailyotengenezwa nchini Korea Kusini ni ya viwango vy ahalio ya juu. Abirfia wanaosubiri kwa hamu kuanza kwa safari za ‘ Deluxe Train’ wajiandae kusafiri kwa raha na wavipuuze vyombo vya habari ambavyo kwa makusudi vinapotosha umma.
Karibuni tupande treni ya Deluxe kwenda Kigoma Aprili 01 , 2015 tuone ukweli halisi.
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu Dar es Salaam,
Machi 11, 2015
0 comments