Monday, 9 March 2015

WAKILI: PONDA HANA KESI YA KUJIBU

By    

UPANDE wa Utetezi dhidi ya Kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Shekh Ponda Issa Ponda umesema kuwa Kiongozi huyo hana kesi ya kujibu kutokana na udhaifu uliopo katika hati ya Mashitaka pamoja na Mashahidi wake

Taarifa hiyo ambayo imetolewa Hayo na Mawakili upande wa utetezi wakati wakiwasilisha hoja ya kutaka kuona Kiongozi huyo hana hatia katika mahakama ya Hakimu Mkoani Morogoro

Akizungumza na dira ya habari mara baada ya kumaliza kutoa hoja hizo Wakili wa Sheikh Ponda Juma Nassoro amesema kuwa upande wa Mashitaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha dhidi ya Kiongozi huyo

Aidha Juma Nassoro ameweza kuzungumzia hoja ambayo waliitoa kuonyesha kuna udhaifu wa mashahidi kutoka upande mashitaka

Hata hivyo mahakama ya hakimu Mkoani Morogoro umeiharisha kesi hiyo hadi machi 20,mwaka hu ili upande wa mashitaka kuweza kujibu hoja hizo.

CHANZO:  Radio Imaan

0 comments