Friday, 20 March 2015

WANASHERIA: VIONGOZI WENYE KAULI YA KUUDHI WAAJIBISHWE

By    

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema ipo haja ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma kutekelezwa kama ilivyoainishwa na sekretarieti na endapo wapo viongozi wanaotoa kauli zenye kuudhi wawajibishwe.

Aidha kimesisitiza haja ya kuheshimiwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 hususani ibara ya 132.

Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urio alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumzia mwenendo na hatua za kisheria kwa viongozi wa umma wanaokiuka maadili na kuongeza kuwa ifahamike kuwa Mahakama Kuu ni chombo cha mwisho cha utoaji haki kwa pamoja na Sekretarieti ya Maadili ambavyo haviingiliani.

0 comments